Na Mwandishi Wetu
Wanachama wa mfuko wa penseni wa LAPF kunufaika na fao jipya lilozinduliwa hivi karibuni nchini kwa Baraka zake Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI Mh. Hawa Ghasia. Fao hilo lijulikanalo kama ‘Piga Kitabu na LAPF’ limelenga kuwakopesha wanachama wa LAPF mikopo ya elimu ya juu kwani ni ombi la muda mrefu kutoka kwa wanachama wa mfuko huo. Hivyo kwa kuthamini na kuona umuhimu wa elimu Mfuko wa Penseni wa LAPF umjibu kiu yao ya muda mrefu ili kumpunguzia mzigo mwajiri.

Akizungumza
kutoka Dodoma, Mkurugenzi Mkuu wa LAPF Bwana Eliud Sanga alieleza
kuwa mfuko wa Pensheni wa LAPF una
huduma nyingi na ambazo zimelengwa kwa ajili ya jamii na hususani zinazochangia
sana kwenye maendeleo. “Huduma hii mpya ya Fao la Elimu imetengewa shilingi
Bilioni Tatu (3) kwa mwaka huu wa fedha ikiwa ni kianzio cha mfuko huu,
tunaahidi mwaka unaofuata fao hili litatengewa bajeti kubwa zaidi kutokana na
umuhimu wake katika nchi yetu, wanachama wengi wameshanufaika mpaka sasa na
wengine wengi zaidi wanazidi kutuma maombi ya kupata mkopo wa elimu ya juu. Fao
hili litawanufaisha wanachama maelfu na maelfu, wanachama wengi watume maombi
kunufaika na huduma hii”
“Mwanachama
anatakiwa kujaza fomu ya mkopo wa elimu LAPF/LON.2, ambayo hupatikana katika
ofisi zote za LAPF pamoja na ofisi za waajiri wachangiaji na pia kwenye tovuti
ya LAPF www.lapf.or.tz. Baada ya
kukamilisha fomu na kuambatisha vielelezo vinavyotakiwa atawasilisha fomu hiyo
kwenye ofisi za LAPF au atatuma kwa njia ya posta. Fao hili la Mkopo wa Elimu
kwa mwanachama utalipwa moja kwa moja chuoni kila mwaka wa masomo kwa taratibu
za chuo husika na urejeshaji wake utakuwa kwa muda wa miaka mitano tangu
ulipoanza kutolewa” Aliongeza Bwana Sanga.
‘Piga Kitabu na LAPF’ ni fao la elimu
litakalotolewa kwa mwanachama yoyote wa
lapf ambaye amekidhi vigezo kama kupata kibali cha kusoma toka kwa mwajiri
wake, barua (admission letter) ya kukubalika kujiunga na chuo cha hapa nchini
kilichosajiliwa na nacte au tcu na awa na michango inayozidi kiasi cha mkopo
unachoombwa kwa asilimia 25.
No comments:
Post a Comment