KAMPUNI ya
kufua umeme ya Pan African Power Solution inayoimiliki kampuni ya Independent
Power Tanzania Limited (IPTL) imezidi kung’aa katika nchi za jumuia ya Afrika
Mashariki katika kusambaza nishati ya
umeme.
Hatua hiyo
inasababishwa na serikali ya Kenya kuipatia barua kampuni hiyo ya kufanya nao
kazi ya usambazaji umeme katika mradi unaohusisha nchi mbili za jumuia hiyo,
ambazo ni Tanzania na Kenya.
Barua ya
Kenya iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Petroli, Injinia
Joseph .K. Njoroge ya tarehe 19, Agosti 2014 kwenda kwa Mwenyekiti Mtendaji wa
PAP, Harbinder Sing Sethi.
Taarifa
zaidi kuhusiana na barua hiyo, yenye kumbukumbu namba ME&D/CONF/3/2/73A iliyokuwa na kichwa cha habari Expression
of interest for IPP for 2000MV power generations and supply to Kenya and
Tanzania.
Barua hiyo,
ilieleza kuwa inazitaka pande tatu hizo ikiwemo PAP, Tanzania na Kenya kukutana
haraka kuona ni namna gani uzalishaji huo utaanza haraka iwezekanavyo.
Akithibitisha
barua hiyo, Katibu na Mwanasheria Mkuu wa IPTL/PAP, Joseph Makandege alisema
kampuni yao inaendelea kuchapa kazi na haitishiki na kauli za wanasiasa kwa
kuwa wao si wanasiasa.
‘’Tunafurahi
kuwa tunazidi kuaminiwa na serikali mbalimbali ndani na nje ya Tanzania. Hii
inadhirisha ufanisi na ueledi wetu katika tasnia nzima ya nishati,’’alisema.
Hivyo,
alisema anaamini maneno yote yanayoenezwa juu yao kuwa yanatawaliwa na chuki na
wivu wa kibiashara kutoka kampuni zingine za usambazaji wa umeme.
Kutolewa kwa
barua hiyo kwa IPTL kutaweza kuondoa sintofahamu iliokuwepo, baada ya Mbunge wa
Kigoma Kusini, David Kafulila(NCCR- Mageuzi) kudai kuwa Seth anayeongoza
kampuni hiyo amepigwa marufuku kufanya biashara ya aina yoyote Kenya.
Kafulila
alinukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini hapa, kuwa Seth ni fisadi na
kwamba Kamati ya Bunge ya nchini Kenya imempiga marufuku kufanya biashara
nchini humo.
No comments:
Post a Comment