HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 16, 2014

KAMPENI YA MWANAMKE NA UCHUMI SASA KUHAMIA TANGA

 Mkurugenzi wa Angels Moments inayoendesha Kampeni ya Mwanamke na Uchumi, Naima Malima akitoa hotuba ya ufunguzi wa kampeni hiyo iliyofanyika mkoani mwanza hivi karibuni. Kampeni hiyo yenye lengo la kuwawezesha wanawake kiuchumi iliandaliwa na kampuni ya Angels Moments. Picha na Angels Moments.
 Mshairi maarufu bibi sauda akitoa burudani ya mashairi yake adhimu kwa lugha ya kufurahisha na burudani kwa wanawake wajasiliamali katika kampeni ya mwanamke na uchumi jijini mwanza.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilemela ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Kampeni ya Mwanamke na Uchumi iliyofanyika Mwanza, Mh. Amina Masenza akifurahia mashairi ya Bi. Sauda (hayupo pichani) katika kughani mashairi yake kwa lugha ya kiswahili.
Mtoa mada maarufu Emiliani Busara akitoa mada na kufundisha biashara bora kwa wajasiliamali jijini mwanza katika kampeni ya mwanamke na uchumi zilizofanyika jijini mwanza hivi karibuni.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mh. Amina Masenza akihutubia wanawake wajasiliamali katika ufunguzi wa semina za kampeni ya mwanamke na uchumi jijini mwanza hivi karibuni.
mjasiliamali mwenye ulemavu wa macho akiuliza swali kutoka kwa watoa mada katika kampeni ya mwanamke na uchumi mkoani mwanza.
Mkuu wa Wilaya ya ilemela Mh: Amina Masenza  bidhaa za wajasiliamali katika moja ya mabanda ya wanawake
walioshiriki katika kampeni ya mwanamke na uchumi katika viwanja vya magomeni kirumba jijini mwanza.
Huduma za upimaji Afya zilitolewa  kwenye kampeni ya mwanamke na uchumi inayotolewa na kampuni ya Angels Moments jijini mwanza hivi karibuni.
Balozi wa kampeni ya mwanamke na uchumi, Linah Sanga akitoa burudani katika ufunguzi wa kampeni ya mwanamke na uchumi mkoani mwanza.
Picha ya pamoja. 


Na Mwandishi Wetu

Baada ya kutoa  elimu juu ya mafanikio na ujuzi wa biashara na ujasiriamali kwa wanawake wajasiriamali mkoani Mwanza, kampeni ya mwanamke na uchumi inahamia mkoani Tanga ambapo wanawake na vijana zaidi ya 600 wanategemea kupata elimu ya msingi juu ya ujasiliamali na fursa zilizopo na nidhamu ya matumizi katika kuhifadhi fedha na mikopo.



“Sasa tunahamia mkoa wa Tanga ambapo sasa mafanikio ya kampeni ya mwanamke na uchumi tunayapeleka kwa wanawake wajasiliamali na vijana ambapo pamoja na mambo mengine,tumefanya tathimini ya mkoa wa Mwanza imeonesha mafanikio makubwa kwani mrejesho ni mkubwa na hamasa ni ya kutosha ambapo wajasiriamali wanatuomba turudi tena, na hili ni jambo la kutia moyo”Anasema Naima Malima Mkurugenzi wa Angels Moment waratibu wa kampeni ya mwanamke na uchumi kwa wanawake wajasiriamali nchini.



“Unajua mkoa wa Tanga unafursa nyingi sana,na jambo la kufurahisha ni kwamba viongozi wengi wa mkoa huu ni wanawake kama mimi, ukianzia mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya wote ni wanawake na wanajitahidi kuhakikisha wajasiliamali wanasonga mbele ambapo pamoja na mambo mengine masuala haya yatajadiliwa na kufundishwa na wataalamu na watoa mada hivyo elimu ya ujasiliamali na fursa zilizopo, usimamizi binafsi wa fedha na uwekaji akiba, afya bora na uchumi kwa akina mama na mwisho ni mwanamke na rslimali ardhi tunategemea mada hizi zitafundishwa kwa usitaadi wa hali ya juu na wakufunzi wetu” anasisitiza Mkurugenzi huyo.



Kampeni ya mwanamke na uchumi mkoani Tanga inatazamiwa kuhudhuliwa na wawezeshaji na wakufunzi maarufu kama ndugu Emiliani Busara na Bi. Tabu Likoko kutoka taasisi ya WAMA ya jijini Dar es Salaam. Elimu sahihi juu ya mada tajwa hapo juu zitatolewa ambapo wanawake wajasiriamali kutoka wilaya za Tanga, Muheza, Mkinga na Pangani zitashiriki.

Kampeni hii ni ya pili kufanyika katika mkoa wa Tanga,baada ya awali kufanyika mkoani Mwanza ambapo itapambwa na Balozi wa kampeni ya mwanamke na uchumi Mwanamziki LINAH SANGA ambaye ataburudisha na kutoa elimu kupitia mziki wake na wimbo maalumu wa kampeni ya mwanamke na uchumi ambapo imepanga kufanyika terehe 10 na 11 mwezi ujao jijini Tanga.

No comments:

Post a Comment

Pages