Aliyekuwa mjumbe wa Kamati ya Umoja wa Vijana Msikiti wa
Mtambani, Hassan Hussein akionyesha darasa lililoungua na moto katika Shule ya Sekondari
ya Seminari ya Mivumoni jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)
Askari Polisi akihakikisha usalama unakuwepo wakati wa zoezi la kuzima moto katika Msikiti wa Mtambani.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura (wa pili kulia) akitoka katika Msikiti wa Mtambani jijini Dar es Salaam, ambapo moto ulizuka katika ghorofa ya pili katika Shule ya Sekondari ya Mivumoni.
Dar es Salaam, Tanzania
Dar es Salaam, Tanzania
MSIKITI wa Mtambani, Manispaa ya Kinondoni, jijini Dar es
Salaam, umeungua moto ikiwa ni awamu ya pili ambapo Agosti 13, mwaka huu
uliungua.
Kwa mara ya kwanza msikiti huo uliuungua katika ghorofa ya
juu na kuteketeza eneo kubwa ambalo hadi sasa bado halijanza
Ghafla jana ulizuka Akizungumza na waandishi wa habari,Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius
Wambura, alisema kuwa chanzo cha moto
huo bado hakijafahamika.
Kamanda Wambura alisema kuwa moto huo unasadikika kuanza majira ya saa 6:30
mchana katika moja ya chumba ambacho wanafunzi wa kike wa kidato cha nne waliokuwa
wamepiga kambi ya kujisomea ili kukabiliana na maandalizi ya mtihani wa Taifa utakaofanyika
baadaye mwaka huu.
humba ambacho moto ulianzia ni chumba cha wasichana na
magodoro manne yameungua.
“Katika janga la moto uliounguza madarasa mwezi uliopita
Jeshi la Polisi liliiunda timu ambayo ilikuwa ikichunguza chanzo cha moto huo
hivyo timu hiyo itaendele na uchunguzi wake kwa kuunganisha matukio haya
mawili” alisema Wambura.
No comments:
Post a Comment