Meneja wa Bia ya Ndovu Special
Malt, Pamela Kikula akikambidhi, Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa
(Tanapa), Pascal Shelutete darubini 20 pamoja na vifaa makini vya utambuzi wa mahali
walipo tembo ili kuwalinda na majangili.
Katikati ni Mkuu wa Idara ya Ulinzi Serengeti, Agricola Roman. Hafla
hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)
Meneja wa Bia ya Ndovu Special
Malt, Pamela Kikula (kulia),
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa), Pascal Shelutete na Mkuu wa Idara ya Ulinzi Serengeti, Agricola Roman wakionesha darubini 20 pamoja na vifaa makini vya utambuzi wa mahali walipo tembo ili kuwalinda na majangili. Katikati ni Mkuu wa Idara ya Ulinzi Serengeti, Agricola Roman.

Malt, Pamela Kikula akizungumza katika hafla hiyo.
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa
(Tanapa), Pascal Shelutete akizungumza kabla ya kupokea darubini 20 pamoja na vifaa makini vya utambuzi wa mahali
walipo tembo ili kuwalinda na majangili kutoka TBL. Kulia ni
Meneja wa Bia ya Ndovu Special
Malt, Pamela Kikula
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Bia maarufu ya Ndovu Special Malt leo imefungua ukurasa
mwingine ikiwa ni muendelezo wa harakati zake za kusaidia kuimarisha ulinzi wa
Tembo wetu hapa nchini. Bia hii ya Ndovu Special Malt ambayo pia imebeba jina
la mnyama huyu adhimu “Ndovu” anayekabiliwa na tishio kubwa la kutoweka duniani
kufuatia uwindaji haramu na ujangili uliokithiri, imedhamiria kufanya kila
linalowezekana katika kumlinda mnyama huyu.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini
dar es salaam, Meneja wa Bia ya Ndovu Bi. Pamela Kikuli alisema Bia ya Ndovu
Special Malt imeweka mikakati na dhamira kubwa kuhakikisha tunamlinda mnyama
huyu Tembo kwa njia yoyote ile. Huu ni urithi wetu na vizazi vijavyo, na pia ni
fahari ya Taifa letu kama ilivyo bia hii ya Ndovu, hivyo tukiacha mnyama huyu
akatoweka tutapoteza fahari ya taifa letu na urithi wetu.
Kwa kulitambua hilo,
Bia ya Ndovu imeamua kuwa mstari wa mbele kuhakikisha Tembo wetu wanalindwa kwa
kila itakavyowezekana. Kama mtakumbuka mwaka jana bia ya Ndovu iliendesha
kampeni ya kumlinda tembo dhidi ya majangiri kupitia mitandao ya kijamii na
kuwazawadia watu walioshiriki katika kampeni hiyo zawadi ya kwenda kujionea
makundi ya Tembo katika hifadhi ya Selou na kusaidia Asasi moja inayojihusisha
na ulinzi wa Tembo.
Mwaka huu tumekwenda mbali zaidi na kuamua kutoa vifaa
muhimu kabisa vinavyosaidia katika ulinzi wa Tembo wetu, tunatoa viona mbali au
Darubini (Binoculars) 20 na vifaa makini vya utambuzi wa mahala walipo tembo (Trimble
GPS) 5, ili kuimarisha doria dhidi ya majangiri hawa. Tuna imani kubwa kuwa
vifaa hivi vitasaidia sana katika ulinzi wa Tembo wetu na hivyo kutimiza
malengo yetu. Alisema Pamela.
Akiongelea juu ya
hatari inayolikumba taifa letu kwa jinsi Tembo wanavyoteketea kwa kasi Pamela
alisema; TBL tumeona jinsi Tembo wetu wanavyoteketea kwa kasi hapa Tanzania na
Afrika kwa ujumla, ili kuokoa hali hii tukaipa jukumu Bia yetu iliyobeba jina
hili lenye ufahari wa pekee, bia ya Ndovu kuchukua jukumu la ulinzi wa myama
huyu. Katika kutekeleza hayo tunawashirikisha wananchi na wapenzi wa bia hii
katika zoezi hili kupitia mitandao ya kijamii. Mwaka huu tumeshirikiana na
uongozi wa TANAPA na wenzetu wa Serengeti National Park kuona ni jinsi gani
tutaimarisha doria katika hifadhi zetu. Na tunaahidi kuwa kampeni hii ni
endelevu hadi tuhakikishe mafanikio yamepatikana.
Naye Meneja Mawasiliano wa Tanapa Bw. Pascal Shelutete
alisema; TBL kupitia bia yake hii ya Ndovu Special Malt, imekuwa mstari wa
mbele katika ulinzi wa Tembo wetu.
Wote sisi ni mashuhuda wa mchango ambao Bia ya Ndovu inautoa katika kuhakikisha Tembo wetu wanakuwa salama, lakini pia kuwahamasisha watanzania wengine kujenga dhamira ya kuwalinda wanyama hawa wakubwa, wapole na wa kuvutia. Vifaa walivyotupatia leo, ni miongoni mwa vifaa muhimu sana katika ulinzi wa wanyama wetu. Hivyo tunawashukuru sana na kuomba waendelee na moyo wao huu wa kizalendo. Nichukue nafasi hii pia kuwaomba makampuni na taasisi nyingine kuiga mfano huu bora wa TBL.

Nae mkuu wa kitengo cha kudhibiti ujangili toka hifadhi
ya Serengeti, Bw. Agrikola Luhiru alisema; vifaa hivi ni muhimu sana katika
doria zetu, vinarahisisha kazi yetu na kutupa uwezo wa kutambua walipo tembo
muda wowote na kuweza kuwafuatilia kwa umakini. Lakini pia kuwaona majangiri
hata kama watakuwa umbali mrefu na kuwadhibiti. Tunaahidi kuvitumia vifaa hivi
kwa malengo yaliyokusudiwa na si
vinginevyo.
Nami napenda niongeze shukurani zangu za dhati kwa niaba ya hifadhi ya Serengeti kwa wenzetu hawa wa Ndovu Special Malt kwa dhamira hii nzuri ya kulinda Tembo wetu. Alisema Luhiru.
Nami napenda niongeze shukurani zangu za dhati kwa niaba ya hifadhi ya Serengeti kwa wenzetu hawa wa Ndovu Special Malt kwa dhamira hii nzuri ya kulinda Tembo wetu. Alisema Luhiru.
No comments:
Post a Comment