HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 24, 2014

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA KONGAMANO LA WAKAGUZI WA HESABU ZA NDANI

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua Kongamano la mwaka la siku tatu la Wakaguzi wa Hesabu za Ndani, linaloendelea kwenye ukumbi wa mikutano wa AICC jijini Arusha. Kongamano hilo limefunguliwa leo Septemba 24, 2014. Picha na OMR.
Baadhi ya washiriki waliohudhuria Kongamano hilo, wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akihutubia katika ukumbi wa AICC jijini Arusha.

 Mahmoud Ahmad, Arusha
Serekali imewataka wakaguzi wa ndani kufanyakazi zao kwa uhuru ilikuisaidia serekali katika kuleta maendeleo na ufanisi, kwani bila  wao zoezi zima la kujipatia maendeleo na uwajibikaji katika taasisi litakuwa halina uwazi na uhuru hivyo kutoweza kuisaidia serekali.

Kauli hiyo imetolewa leo katika mkutano wa wakaguzi wa ndani uliofunguliwa na makamu wa raisi Dkt Gharibu mohammed Bilal jijini hapa huku akiwataka kufanyakazi zao kwa ufanisi ilikuleta tija kwa taifa.

Dkt Bilal alisema kuwa ilikuwa na maendeleo tunahitaji kuwa na wakaguzi waliohuru kufanyazi na kukagua sekta zima pamoja na kutoa ushauri bila ya kuwa na kizuizi chochote ndio maana serekali ikaweka ofisi ya mkaguzi mkuu wa ndani.

Aliwataka wakaguzi kujishughulisha na kazi zote za ukaguzi bila ya kuchagua kazi mojawapo ilikuweza kuisaidia serekali kwenye idara mbalimbali walizopo na kuwa wao si wa eneo moja pekee.

Pia aliwataka kujifunza kutoka kwa wakaguzi wan je na wa ndani waliohudhuria mkutano huo ilikuendana na kazi yao kwa ni muhimu kwa maendeleo na kuwa wanaokaguliwa wanahitajika kutoa mashirikiano kwa wakaguzi hao wa ndani.

“Wakaguzi wawehuru kusema mambo yalivyondani ya taasisi ilikuleta ufanisi bila ya kuwa na woga kwani wao ndio walinzi wa taasisi zetu na kuwa watoe usharui nini kinatakiwa kifanyike ilikuweza kuleta ufanisi katika taasisi”alisema dkt Bilal.

Nae raisi wa taasisi ya wakaguzi wa ndani Emmanuel Johannes alisema kuwa sekta ya wakaguzi inachangamoto kubwa ya kukabiliana na mifumo ya kiserekali kwa kutofanyakazi zao kwa uhuru hivyo akawataka wanaokaguliwa kuwapa ushirikiano iliwaweze kutimiza majukumu yao.

Johannes alisema kuwa wakaguliwa watakapowapa ushirikiano na kukubali ushauri wataisaidia kupunguza manunguniko yanayoendelea ikiwemo ya ufisadi na kuwa kutakuwa na uwazi katika setka mbalimbali na taasisi zake.

Alisema kuwa wao ni sehemu ya waangalizi wa matumizi ya rasilimali za taasisi jinsi zinavyowanufaisha wananchi ikiwemo kukua kwa uwajibika na utawala bora ndani ya taasisi hizo hivyo wanawajibu mkubwa kuhakikisha mazingira ya kazi zao yanakuwa na uhuru.

Aidha mkuu wa mkoa wa Arusha Magessa Mulongo aliwataka wakaguzi wa ndani kutambua majukumu yao na kuyatekeleza kwa uhuru bila ya kuangalia ukubwa wa tatizo na kutoa ushauri utakosaidi ukuaji wa uchumi.

Mulongo alisema kuwa ni vyema wakaguzi wakatambua misingi ya sheria za ukaguzi na kuzifanyiakazi ilikuondokana na manung’uniko yanayoendelea hivi sasa hapa nchini ikiwemo suala la ufisadi,matumizi mabaya ya madaraka,na rasilimali za nchi.

No comments:

Post a Comment

Pages