Baadhi
ya Ombaomba waliokutwa na Mwandishi wakiomba kwenye mitaa mkoani Dodoma.
Na Bryceson Mathias, Dodoma
Na Bryceson Mathias, Dodoma
WAKATI Tatizo la Ombamba nchini likiwa Sugu na jitihada za kulitatua bado hazijafanikiwa; Ombaomba mkoani Dodoma wamesema, Ijumaa yoyote kwao kama ilivyo jana, kwao ni Siku yao ya Mshahara (Payday), hivyo wanawataka Watendaji wa Halmashauri Dodoma wasiwabughudhi.
Wakizungumza wakiwa kwenye msururu wa kugawiwa 'Uji na Unga kibaba kimoja mkoani hapa jana, pembeni kidogo mwa Msikiti wa Nunge karibu na Hotel ya Wimpy, Ombaomba hao walidai, wanataka wasibughudhiwe kwa sababu siku hiyo ni siku ya malipo na mshahara kwao.
Walipoulizwa ni nani anayewalipa Mshahara wakati hawafanyi kazi ila kuomba, walijigamba wakisema kama wafanyakazi wengine wanavyolipwa na waajiri wao, nao wana Waajiri wao barabarani ambapo watu wenye mapenzi mema na roho nzuri, huwapatia chochote walichonacho.
“Kama ninyi mnavyodai na kuandamana mnapocheleweshewa mishahara, hata sisi siku ya Ijumaa ambapo Wa-Islamu na watu wenye mapenzi mema, hutupatia zaka zao ikiwa ni pamoja na Chakula, Fedha na Nguo, siku hiyo ikichelewa huwa tunakaribia kuwaandamia.
Tunawashangaa sana Askari na Wafanyakazi wa Halmashauri ya Mji wa Dodoma wanapotuondoa barababarani wakati tupo kwenye meli moja ya kujitafutia riziki! Tofauti yetu ni kwamba, wao wanaomba kwa kufanya kazi, sisi tunaomba kwa kusaidiwa”.alisema Mama aliyejita Mdala Roda.
Utafiti uliofanywa 2013 na Shirika linashughulika na masuala ya Familia na Afya (FHI360) chini ya mradi wa Pamoja Tuwalee; Kati ya watoto 332 waliohojiwa, asilimia 35.5 sawa na watoto 118, walibainika wanatoka Dodoma; Ingawa watendaji wake wanalifumbia macho.
Awali katka tathimini ya Julai 31, 2013 Afisa Mwandamizi wa Shirika hilo, Judith Masasi, aliyekuwa Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Victoria Bura, alisema ipo haja ya nguvu kubwa kuelekezwa kwa watoto wa aina hiyo ili kuwasaidia na kuokoa kizazi kijacho.
No comments:
Post a Comment