Sam Mapenzi, Joniko Flower na Hashim Donode wakiwapa raha mashabiki wa Skylight Band kwenye Nyama Choma Festival iliyofanyika miwshoni mwa juma katika viwanja vya michezo vya chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Mashabiki wakiwa wameshona kwenye viwanja vya michezo vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika Nyama Choma Festival huku Skylight Band wakitoa burudani ya aina yake.
Nyomi la kufa mtu... hapa chezea Skylight Band ndio habari ya mujini kwa sasa.
Mashabiki wa Skylight Band wakijiachia kwa raha zao.
Mmoja wa mashabiki akiwa ameshika kiuno kuhamaki kwa kile anachokiona jukwaani kutoka kwa Skylight Band kwenye tamasha la Nyama Choma.
Aneth Kushaba AK47 akiwapa vionjo vya aina yake mashabiki wa Skylight Band kwenye tamasha la Nyama Choma.
Digna Mbepera wa Skylight Band akifanya yake jukwaani kwenye tamasha la Nyama Choma.
Sam Mapenzi akiporomosha mistari kwa mashabiki wa Skylight Band Nyama Choma Festival.
Sony Masamba akiwachizisha mashabiki wa Skylight Band Nyama Choma Festival.
Wapiga vyombo wa Skylight Band wakiwajibika kuhakikisha mashabiki wanapata kitu roho inapenda.
No comments:
Post a Comment