HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 09, 2014

Villa Squad kukipiga na Ashanti United

Na Andrew Chale

Kwa mujibu wa  Katibu wa Villa, Mbarouk Kasanda  mchezo huo utakuwa ni mahususi kwa ajili ya kukipa makali kikosi chao hicho kinachotarajia kujiwinda kurejea ligi kuu msimu ujao.

Kasanda aliwaomba  marafiki wa Villa na wadau wa soka Kinondoni kujitokeza kwa wingi  uwanja wa shule ya Msingi Mwananyamala kushuhudia timu hiyo yenye wachezaji mbalimbali wakiwemo walioachwa na timu kubwa zikiwemo za Simba, Yanga, Azam, Mtibwa na Coastal Union. 
Mcheazo huo unatarajiwa kuwa mkali kwa timu zote mbili, kutokana na kukamiana kila wanapokutana, ikiwemo zilipokuwa ligi kuu misimu iliyopita. Kiingilio cha mchezo  huo kinatarajiwa kuwa sh 1,000.
Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Villa, Idd Godgod alisema wameamua kujipanga kuakikisha wanarejea ligi kuu ndio maana wamesajili wachezaji wakongwe na wazoefu sambamba na kuchanganya damu changa.
Godgod aliwataja baadhi ya wachezaji waliowasajili  chini ya ufadhili wa mdau wa soka, Nassoro Binslum, ni pamoja na Ramadhani Chombo ‘Redondo’ aliyeachwa na Simba, Ibrahim Mwaipopo kutoka Azam FC na Ally Mohamed ‘Gaucho’ (Mtibwa Sugar)  ya Morogoro.
 Wengine ni Nurdin Bakari, Godfrey Taita, Pius Kasambale,Jamal Magulu, Rashid Roshuwa na wengine wengi ambao kwa sasa bado wanasubiria hatua ya mwisho kuwaweka wazi.
Pia timu hiyo inatarajia kuendelea na mazoezi yake uwanja wa Muhimbili chini ya kocha wao, Kamba Lufu ambapo wadau mbalimbali wameombwa kujitokeza kuipa sapoti timu hiyo.

No comments:

Post a Comment

Pages