Meneja wa Masoko na mawasiliano
wa taasisi ya kifedha ya Bayport Tanzania, Ngula Cheyo (katikati) akiongea na
wandishi wa habari (Hawapo pichani) wakati wa utambulisho wa huduma ya Mikopo
ya bidhaa.
Meneja wa Masoko na
mawasiliano wa taasisi ya kifedha ya Bayport Tanzania, Ngula Cheyo (wa kwanza
kushoto), akifuatiwa na Meneja masoko wa
Toyo, Drima Makachwa (katikati) pamoja na
Meneja Bishara wa Bayport, Thabit Mndeme (kulia), kwenye uzinduzi huo.
Na Andrew Chale
Taasisi ya kifedha ya Bayport
Tanzania mapema leo Oktoba 15, 2014 imezindua
huduma mpya ijulikanayo kama Mikopo ya bidhaa ikiwa na lengo la kurahisisha
utendaji kazi wa watumishi wa umma na wafanyakazi wote wa kampuni
zilizoidhinishwa na Bayport.
Uzinduzi huo ulifanyika katika ofisi za makao makuu ya
Bayport, maeneo ya Moroco jijini Dar es Salaam mbele ya wandishi wa vyombo
mbalimbali vya habari umeonyesha
matumaini mapya ya watanzania wanaosumbukia usafiri katika vituo vyao vya kazi,
hususani maeneo ya mikoani ambako mara kadhaa kumesikika malalamiko ya maisha
magumu kwa watumishi wa umma.
Akizungumza juu ya tukio
hilo, Meneja Bishara wa taasisi hiyo Thabit Mndeme alisema kwamba ni wakati wa
kukuza uchumi wa nchi kuhakikisha kuwa watu wanafanya kazi kwa bidii na shauku.
Alisema wapo watumishi ambao
wanaishi kwa tabu kutokana na changamoto ya usafiri na mahitaji mengine ya
kijamii ,hivyo kutokana na huduma hiyo mpya ya kukopeshwa pikipiki ,boda boda
itasaidia kwa kiasi chake.
Pia alisema Bay port imekaa
kuangalia namna ganib watanzania wataendelea kufanya kazi kwa moyo na kukuza
uchumi ambao uko sambamba na kuwakopesha
fedha kama wanavyofanya kwa sasa na kuamua kuwakopesha tena na bidhaa za
usafiri.
Naye Meneja wa Masoko na
mawasiliano wa taasisi hiyo Ngula Cheyo alisema kuwa mikopo mipya kwa sasa
inapatikana kwa masaa 24, huku ikipatikana pia kwa mikoa na wilaya zote kwenye
ofisi za Bayport zaidi ya 80, nchini.
Bayport ni Taasisi ya kifedha
isiyo ya kibenki inayoongoza katita utowaji wa mikopo barani Africa na Amerika
ya kusini .imeanzishwa mwaka 2001, na umiliki wake ukiwa Mauritius.
No comments:
Post a Comment