Na Bryceson Mathias, Chibelela, Bahi
KASISI Ujumla (Vicar
General), George Chomola, wa Kanisa la Anglikani Dayosisi ya Central Tanganyika
(DCT) Dodoma, ameililia Katiba Mpya akisema inasumbua kwa sababu hakuna Upendo
miongoni mwa Watendaji wake.
Akizungumza katika
Msiba wa Mjumbe wa Halmashauri Kuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) NEC, Ernest
Masima, aliyezikwa nyumbani kwake katika kijiji cha Chibelela mkoani Dodoma
mwishoni mwa Wiki, Chomola amesema, Katiba Mpya inasumbua kwa sababu hakuna
Upendo.
Ingawa Chomola hakutaka
kuingia ndani ili kufafanua upendo unaokosekana kwenye Katiba mpya
inayopendekezwa, lakini Mizengwe, Kukosekana Maridhiano, Vituko na Udanganyifu
uliokithiri katika upigaji kura wa Bunge Maalum la Katiba kutafuta Theluthi
Mbili ni mojawapo.
Mbali na kwamba Msiba
huo ulikiumiza CCM kwa jinsi Kada wake Marehemu Ernest alivyokitumikia na
kukisaidia kufanya Mengi ikiwa ni pamoja na Ushauri akiwa Mkuu wa Wilaya na
kazi zingine katika sehemu mbalimbali, CCM isifadhaike, Mungu amempenda zaidi.
Kasisi Chomola alinukuu
Neno la Mungu la Yohana 14:1-2 kuwafariji CCM, Ndugu na Waombolezaji
linalosema, “Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi.Nyumbani
mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia………;”
Kwetu sisi kwa Upande
wa Kanisa tuna Majonzi Makubwa kwa sababu alikuwa Kiongozi wa Shughuli
mbalimbali za Kanisa ikiwa ni pamoja na Ujenzi wa Kanisa la Anglikani hapa
Chibelela, lakini bado nasema Mungu anasema, ‘Msifadhaike’”.alisema Chomola.
Hata hivyo, Chomola
Kabla ya kutoa Mahubiri, alimkaribisha Katibu wa CCM Mstafu Yusuf Makamba ili
aelezee anavyomfahamu Marehemu, lakini alimpiga ‘Stop’ asije akaanza sihubiri, akidai
hasa kutokana na kwamba anafahamu vifungu vingi vya Neno la Mungu.
No comments:
Post a Comment