Katibu Mkuu
Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Alhaji Yusuf Makamba akiwa kwenye Msiba
wa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Ernest Masima kijijini kwake Chibelela.
Na Bryceson Mathias,
Chibelela Bahi
KASISI Ujumla (Vicar
General), George Chomola, wa Kanisa la Anglikani Dayosisi ya Central Tanganyika
(DCT) Dodoma, Jumapili Oktoba 12, katika Kijiji
cha Chibelela, alimpiga ‘Stop’ Katibu Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Alhaji
Yusuf Makamba, asihubiri kwenye Msiba wa, Ernest Masima,.
Akizungumza kabla ya kutoa
Mahubiri ya Neno la Mungu alilolisoma, Chomola ambaye ni Kasisi wa Ujumla wa
Makasisi wa Kanisa hilo mkoani Dodoma alisema, “Nimemuona Alhaji Makamba, tafadhali
tumia dakika Moja utoe Salamu za Rambirambi kwa Waombolezaji, ‘ila Usihubiri’.
Pamoja na kupigwa ‘Stop’
Makamba hakukidhi Marufuku hiyo ya kutumia dakika moja na badala yake alitumia
dakika tatu, akielezea Jinsi ambavyo walifanya kazi na Marehemu ambaye hadi
kifo chake alikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC).
Viongozi mbalimbali wa
CCM akiwemo Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu, Samwel John
Malecela, ambaye alituma salamu za Sauti toka nje ya aliko, walieleza jinsi
ambavyo CCM kimempoteza mtu kiliyemtegemea katika kuimarisha Chama na Ushauri,
Katibu Mkuu wa Wizara
ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Job Masima, amabaye ni mdogo wake na
Marehemu alisema, “Ukiona Paka anamkejeli Paka ujue yuko karibu na Shimo;
Familia kwa Muda mrefu tulijivua Kaka yetu, ambaye muda mwingi aliutumia kwenye
siasa, ingawa mimi siwezi na simfikii.
“CCM kimempoteza Mtu
makini, Jamii imempoteza Mshauri, Kanisa limempoteza Mtendaji, na sisi Familia
tumempoteza Jembe, kwa sababu alikuwa akila Pilipili (Mambo Magumu) kama
anakula asali (akiyafanya mepesi,
Aidha Mdogo mwingine wa
Marehemu, Mchungaji, Noah Masima,
aliuomba radhi umati wa waombolezaji uliohudhuria mazishi hao akisema, “Mtusamehe,
sisi familia, tulikuwa tukishindana wenye kwa wenyewe kuhusu kukosekana kwa
marehemu nyumbani, kumbe alikuwa akiwatumia ‘tumewaona’.
No comments:
Post a Comment