Meneja Mwandamizi wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF)
Kanda yaMagharibi – Tabora, Emmanuel Adina akifafanua jambo kwa mwandishi wa habari (hayupo pichani)
kuhusu Maonyesho ya Wiki
ya Vijana inayofanyika Kitaifa MkoaniTabora.
Afisa Masoko na Elimu kwa Umma wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Bibi Catherine Kameka akielezea jambo kuhusu Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwa wananchi waliotembelea banda lao wakati wa Maonyesho ya Wiki ya Vijana yanayofanyika Kitaifa MkoaniTabora.
MenejaMwandamiziwaMfukowaBimayaAfya (NHIF) Kanda ya Magharibi –Tabora, Emmanuel Adina (kushoto) akifafanua jambo kwa Afisa Habari wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Jonas Kamaleki alipofanya mahojiahano naye kuhusu Mfuko wa Afya ya Jamii unavyonufaisha Vijana wakati wa Maonyesho ya Wiki yaVijana inayofanyika Kitaifa MkoaniTabora
Baadhi ya wananchi wakipata huduma ya upimaji wa Afya inayotolewa bure na Mfuko waTaifa wa Bima ya Afya (NHIF) katika Maonyesho ya Wiki yaVijana yanayoendelea mjiniTabora.
Baadhi ya wananchi wakipata huduma ya upimaji wa Afya inayotolewa bure na Mfuko waTaifa wa Bima ya Afya (NHIF) katika Maonyesho ya Wiki yaVijana yanayoendelea mjiniTabora.
Pichana Frank Shija, Tabora.
Na
Jonas Kamaleki, Tabora
Viongozi wa dini mkoani Tabora wametoa mchango mkubwa katika kuhamasisha
waumini wao kujiungana Mfuko wa Afya wa Jamii (CHF)
na kuufanya mkoa huo kuwa katika hali nzuri ya watu wake kupata matibabu.
Hayo yamebainishwa na
Meneja Mwandamizi wa Mfuko waTaifawa Bima ya Afya (NHIF) Kanda ya
Magharibi-Tabora, Emmanuel Adina katika Maonyesho ya WikiyaVijana
yanayofanyika Kitaifa mjiniTabora.
Adina ameongeza kuwa
viongozi wa dini zote wamekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha waumini wao kujiunga
na CHF ilikuwa na uhakika wa kupata huduma stahiki ya matibabu.
Aidha amesema kuwa viongozi
hao wamekuwa wakihamasisha watu wao misikitini, kwa upande wa Waislam na makanisani
kwa Wakristo. Hadi sasa jumlaya kaya 38,000 wamejiunga na Mfuko huo huku lengo likiwa
ni kufikia asilimia 30 ya waliojiunga na CHF ifikapo Juni 2015, Meneja huyo ameitaja wilaya
ya Igunga kuongoza katika uhamasishaji wa wananchi kujiungana CHF.
“Namshukuru sana Mkuu
wa Wilaya ya Igunga, Bw. Elibariki Kingu kwa mchango mkubwa anaoutoa kwa wanaIgunga
kujinga na Mfuko huo ambapo jumlaya kaya 9,000 wilayani Igunga zimejiunga na
CHF ambayo ni idadi kubwa kutokana na uhamasishaji wa Mkuu wa wilaya”. Alisema, Adina.
Ameongeza kuwa Bw.
Adina amezitaja wilaya nyingine ambazo kaya nyingi zimejiunga na Mfuko huo kuwa
ni Nzega, Uyui, Urambo na Sikonge.
Katikawilayahizokinachosaidiazaidiwatukujiunganikuwepowilayanihumovyamavyaushirikavyamsingivyatumbaku.
Zipopiachangamoto
NHIF inayokutana nazo kuhusiana na wanaTabora kujiungana CHF.
Changamoto hizo Meneja
huyo amezitaja kuwa ni kipato kidogo cha wakazi waTabora inayotokana kuwa
baadhi ya wilaya hazina zao kuu la biashara la kuwapatia kipato cha uhakika,
kutokuwepo na elimu ya kutosha ya mifumo ya Bima na pia ukosefu wadawa na
vifaatiba katika mahospitali, zahanati na vituo vya afya.
Kwa upande mwingine,
Afisa Masoko na Elimu kwa Umma wa NHIF, Bi Catherine Kameka amewataka
wananchi wajiunge kwa wingi na Mfuko wa Afya wa Jamii na Bima ya Afya ili
waepuke usumbufu wa kukosa matibabu wakati wanapokuwa wanahitaji matibabu na
hawana pesa. Amesema ugonjwa hauna msimu, unaweza kujitokeza wakati wowote
hivyo ukiwa kwenye mifumo ya Bima ni rahisi kuhudumiwa.
Ameongeza kuwa huduma
zinazotolewa kwa wanachama wa NHIF zimeboreshwa na kuvutia wanachama wengi
zaidi ikilingani shwa na ilivyokuwa wakati mfuko unaanzishwa. Hivyo amewataka
wana Tabora wachangamkie fursa hiyo ili wawe na afya njema wakati wote kwa
maana mtu akiwa na afya safi anaweza kujishughulisha kikamilifu katika shughuli
za uzalishaji mali.
No comments:
Post a Comment