HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 11, 2014

MASHINDANO YA SHIMISEMITA YAFIKIA KILELE, NSSF YAPONGEZWA KWA KUDHAMINI

Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF)  yadhamini Mashindano ya Shirikisho la Michezo Serikali za Mitaa (Shimisemita) yaliyohitimishwa  rasmi  katika viwanja vya Jamhuri mkoani morogoro. sherehe za  kuhitimisha  zilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Tamisemi Mhe. Agrey Mwanri.

Aidha Waziri wa Tamisemi Mh. Agrey Mwanri amelipongeza Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa kudhamini mashindano hayo na kuleta msisimko mkubwa tangu yalipoanza Novemba 27 ambapo wanamichezo pamoja na watu mbalimbali waliohudhuria mashindano hayo walipata elimu kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na NSSF ikiwemo ya Wakulima Scheme na mpango wa uchangiaji wa Hiari.
 Mgeni rasmi katika mashindano hayo Mhe. Agrey Mwanri ambaye ni Naibu Waziri wa TAMISEMI  akitoa hotuba ya kufunga mashindano hayo katika viwanja vya Jamhuri mkoani Morogoro.
Mhe. Agrey Mwanri ambaye ni Naibu Waziri wa TAMISEMI akikabidhi kikombe kwa nahodha wa timu ya Halmashauri ya Jiji la Tanga baada ya kuibuka washindi wa kwanza katika mchezo wa soka katika mashindano ya Shirikisho la Michezo Serikali za Mitaa (SHIMISEMITA).
 Bondia Francis Cheka akijiandikisha kuwa mwanachama mpya  wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kupitia mpango wa uchangiaji wa Hiari. (HIARI SCHEME)
Ofsa Uhusiano wa NSSF, Aisha Sango akimkabidhi fulana Bondia Francis Cheka baada ya kujiandikisha kuwa mwanachama mpya  wa NSSF katika viwanja vya Jamhuri Mkoani Dodoma.

No comments:

Post a Comment

Pages