Pichani (Katikati) ni Mwanaafa Mwinzagu ambae ni Mshindi wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 akiwa katika Picha ya Pamoja na Baadhi ya wafanyakazi na Wadau wa Kampuni ya Proin Promotions ambao
ndio waandaaji na waendeshaji wa Shindano la TMT mara baada ya
kutangazwa mshindi wa Kitita cha Milioni 50 za Kitanzania katika fainali
ya shindano la TMT lililomalizika Mnamo tarehe 30 Aug 2014 katika
Ukumbi wa Mlimani City na Kumtangaza Mwanaafa Kuwa Mshindi kwa Mwaka
2014.
Na Josephat Lukaza
Mwanaafa Mwinzagu ambae alishiriki Shindano la Tanzania
Movie Talents (TMT) huku akiwa ni Mwanafunzi wa Darasa la Saba katika Shule ya
Msingi Tandika iliyopo Mjini Mtwara katika Manispaa ya Mtwara amefaulu mitihani
yake ya kumaliza elimu ya Msingi Kwa Kupata daraja C huku Masomo ya Hesabu na
Sayansi akiwa kafanya vizuri sana kwa Kupata Daraja B.
Wakati Shindano la TMT lilipofika Mtwara kwaajili ya
kusaka vipaji vya kuigiza Ndipo Mwanaafa alipojiunga na Kuja kushiriki Katika
SHindano hilo Kubwa na lenye mvuto wa Pekee Afrika Mashariki na Kati. Wakati
akihojiwa mara baada ya Kutoka katika hatua ya Kwanza ya Shindano hilo
lililofanyika Mtwara na kuhojiwa Mwanaafa Mwinzago alisema "Hiki ni Kipaji
kwahiyo sina haja ya kuficha na pia naweza Kukosa kwenye Shule nikapata Kwenye
Kuigiza na ndio maana nimekuja Kushiriki" Vilevile alipoulizwa Je Ikitokea
Ukashinda itakuwaje Shule na Sanaa? Alijibu kuwa "Ikitokea nikashinda
katika ngazi ya Kanda ya Kusini Nitaenda Kambini Dar Es Salaam na kuacha Shule
kwanza, Maana Shule Ipo ila Shindano hili linapita tu Kwahiyo Naweza kupata
kwenye Sanaa na nikishinda basi nitarudia Darasa". BOFYA HAPA KUSOMA
ZAIDI»
Mara baada ya Kuibuka MShindi katika Kinyanganyiro Hiko
Katika Ngazi ya Kanda ya Kusini, Timu nzima ya TMT iliweza kumuhoji Mwalimu
wake Mkuu ambapo alisema yafuatayo "Huyu Ni mwanafunzi wa Darasa la Saba
Kwa Sahivi na Hiki pia ni kipaji lakini Sisi kama Wazazi hatuwezi kuzuia Mtoto
kuonyesha Kipaji chake yeye alichofanya alishiriki Mashindano na ameshinda
kwahiyo sisi kama walimu wake tutajadiliana jinsi ya kulitatua hili kwa maana
hatuwezi kujua labda mshindi wa Milioni 50 hatakuwa yeye"
Mara baada ya Shindano la TMT kumalizika tarehe 30 August
2014 wiki moja baadae Mwanaafa aliweza Kurejea Mjini Mtwara kwaajili ya Kufanya
mitihani yake ya Kuhitimu Elimu ya Msingi na Hatimae mara baada ya kuwasili
nyumbani kwao Mwanaafa aliweza kwenda shule kwao kwaajili ya kukamilisha
taratibu za kufanya mtihani na kesho Mwanaafa akaweza kufanya Mitihani yake
vizuri kwa muda wa siku mbili na alipomaliza Alirejea Jijini Dar Es Salaam
ambapo Aliendelea na zoezi la Kurekodi filamu ya Pamoja Ya Washindi wa TMT waliofanikiwa
kuingia Hatua ya Kumi Bora huku yeye akiwa ni kinara katika filamu hiyo ambayo
inatarajiwa kuzinduliwa Mapema Mwezi wa Kumi na Mbili katika Mikoa yote ambayo
TMT ilipita kwaajili ya kusaka Vipaji.
Hapo Majuzi kupitia Vyombo mbalimbali vya habari kupitia
Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) lilitangaza matokeo ya Mitihani ya Elimu ya
Msingi na Ndipo tulipofahamu kuwa Mwanaafa ameweza kujitahidi sana katika
Mitihani huku akiwa kafanya Vizuri sana katika Masomo ya Hesabu na Sayansi
ambapo amepata daraja B huku masomo mengine akiwa amepata daraja C na Kupelekea
kupata wastani wa daraja C.
Kwa Matokeo hayo tunapenda kumpongeza Mwanaafa kwa kuonyesha
uwezo wake katika Masomo na hatimaye kufanya vizuri katika Mitihani yake ya
Mwisho ya Kumaliza Elimu ya Msingi
Ikumbukwe kuwa hapo awali Mwanaafa alisema kuwa endapo
atashinda Milioni 50 katika fainali ya Shindano la TMT lililomalizika tarehe 30
August 2014 basi atatumia Kiasi hiko cha pesa kwaajili ya kujiendelea kielimu
lakini Wakati wa Fainali hiyo Kampuni ya Proin Promotions Ltd iliahidi
kumsomesha Mwanaafa hata Kama asingeshinda katika Shindano hilo.
Kwasasa Mwanaafa yupo chini ya Uangalizi wa Kampuni ya Proin
Promotions ambapo kampuni hiyo itamsomesha Kuanzia Kidato cha Kwanza hadi Cha
Nne.
Kampuni ya Proin Promotions Ltd inapenda kumpongeza Mwanaafa
kwa kufanya Vizuri katika Mitihani yake ya Kumaliza Elimu ya Msingi na
kuonyesha Kuwa Kumbe Bado ni Mshindi hadi Darasani.
No comments:
Post a Comment