Na Hamida Ramadhani, Dodoma
NAIBU Waziri wa Habari Utamaduni na
Michezo Juma Nkamia anatarajia kufunga mashindano ya CESOPE Cup leo katika
uwanja wa Bahi Wilayani Bahi.
Akizungumza na Waandishi wa
Habari, Mkurugenzi wa CESOPE,Anton Lyamunda alisema lengo la Mashindano
hayo ni kutoa elimu ya Mazingira kwa Vijana na kutoa Elimu ya Uraia pamoja na
matumizi ya bwawa la Farkwa
Alisema Mashindano yanaendelea na Mabingwa
katika tarafa 4 za Mndemu,Bahi,Chipanga na Mwitikira zitajipatia Ngombe
na Jembe la kukokotwa na Ng’ombe.
Lyamunda alisema Mashindano hayo
yatagharimu jumla ya shilingi milioni 18.5 huku Bingwa wa Mashindano hayo
akijinyakulia shilingi laki tano wa pili laki tatu na watatu laki mbili.
Alisema kuanzia Novemba 12 mwaka huu
watatoa Elimu kwa siku nne kwa kutumia njia ya Video kwa kuitangaza taasisi na
na hotuba za Baba wa Taifa ili kutoa elimu ya Uraia kwa Vijana kuipenda
Nchi yao.
‘’Tutakuwa na Semina kwa Vijana wa
eneo la Bahi,Mndemu,Chipanga na Mwitikira kwanza ni kuwapa Elimu juu ya Taasisi
yetu na Elimu ya Uraia kwa kupitia hotuba za Baba wa Taifa,’’alisema Lyamunda.
Lyamunda alisema lengo lingine ni
kuwapa nafasi Vijana ambao wapo Vijini waweze kuonekana na kupata nafasi ya
kucheza timu kubwa kwani Soka kwa sasa limekuwa ni Ajira
CESOPE ni Asasi inayojishughulisha
na Utunzaji wa Mazingira na kutoa Elimu ya Uraia kwa kutafuta suluhisho
la kutatua Umaskini na ipo katika Wlaya 3 za Bahi, Manyoni na Chemba.
Wakati huo huo mshambuliaji wa timu ya CDA ‘Watoto
wa Nyumbani’Mohammed Neto amesema atahakikisha anaisaidia timu hiyo ili iweze
kupanda daraja la kwanza na baadae ligi kuu ya Tanzania Bara.
Neto ambaye katika msimu uliopita wa
ligi kuu ya Tanzannia Bara aliitumikia timu ya Mgambo JKT huku katika mchezo
dhidi ya Yanga wa raundi ya kwanza akitolewa kwa kadi nyekundu kutokana na
kuhisiwa kucheza na kitu chenye ncha kali katika uwanja wa CCM Mkwakwani jijini
Tanga
Neto alisema nia yake ni
kuisaidia timu yake katika ligi daraja la pili inayotarajiwa kuanza Novemba 22
mwaka huu huku timu hiyo ikikutana na Mvuvumwa ya Kigoma katika uwanja wa Lake
Tanganyika.
Alisema kutokana na maandalizi
waliyofanya timu hiyo anaamini watairejeshea makali timu hiyo ambayo katika
miaka ya nyuma ilikuwa kiboko ya timu za Simba na Yanga.
‘’Kaka tupo hapa na mchezaji
mwenzangu Iddrisa (Rashid) ambaye nae aliichezea Yanga miaka ya nyuma
tunataka kuirejesha ligi kuu timu hii kwani tuwachezaji wazuri na mwenyekiti
wetu Kaliza (Thadeo)ni mtu wa mpira.
Timu hiyo imepangwa katika kundi A
pamoja na Milambo ya Tabora,Singida United ya Singida,Mpanda United ya Mpanda
na Ujenzi ya Rukwa huku ikitarajiwa kufungua dimba na Mvuvumwa ya Kigoma
Novemba 22 mwaka huu Mkoani Kigoma
No comments:
Post a Comment