Baadhi ya wadau wa muziki wakiwa wamebeba jeneza lililokuwa na mwili wa
mwanamuziki mkongwe wa bendi ya Tabora Jazz, marehemu Shem Karenga wakati wa
maziko yake yaliofanyika leo kwenye makaburi ya Kisutu, jijini Dar es Salaam. (Picha na
Francis Dande)
Ras Inocent Nganyagwa akitafakari jambo wakai wa maziko ya mwanamuzi nguli wa muziki wa dansi marehemu Shem Karenga.
Hassan Rehan Bichuka (kulia) akiwa na wanamuziki wenzake wa zamani wakibadilishana mawazo na Ankal walipokuwana katika maziko ya mwanamuziki nguli wa bendi ya Tabora Jazz, marehemu Shem Karenga.
Ankal akiteta jambo na mwanamuziki mkongwe wa Bendi ya Sikinde Ngoma ya Ukae.
Mwili wa marehemu Shema Karenga ukiwasili katika makaburini ya Kisutu.
Mamia ya waombolezaji wakielekea makaburini.
Mwanamuziki mkongwe Kassim Mapili (katikati) akiwa na wadau wa muziki kulia ni mwanamuziki Tshimanga Asosa na kushoto ni mdau wa muziki Ankal Michuzi.
Mdau wa muziki John Jembele (kushoto) akiwa na Tshimanga Asosa
Na Mwandishi Wetu
Na Mwandishi Wetu
MAMIA ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam na
vitongoji vyake, leo alasiri walijitokeza kumzika nguli wa muziki wa dansi
nchini, Shem Ibrahim Karenga aliyefariki juzi asubuhi na kuzikwa jana alasiri
katika Makaburi ya Kisutu.
Karenga (64), aliyewahi kutamba na bendi
mbalimbali maarufu nchini akianzia Tabora Jazz, alifariki katika akiwa katika hospitali
ya Amana, ambako alilazwa baada ya kukimbizwa Jumapili usiku kutokana na kuzidiwa
ghafla.
Miongoni mwa wanamuziki na wasanii walioshiriki
mazishi ya nguli huyo ni ni mkongwe wa kupiga gitaa Said Mabela, aliyemwelezea
Karenga kama taa ya muzimki wa dansi iliyozimika ghafla.
Mabela alisema, kifo cha Karenga kimemgusa sana
kwani sio tu kama mwanamuziki mwenzake, ni mtu aliyefahamiana naye kwa mufa
mrefu wakati huo akiwa mkoani Kigoma na Bendi ya Ujiji Jazz.
"Karenga ametuachia pengo kubwa katika
tasnia ya muziki wa dansi. Ni mtu aliyeufanyia mengi muziki wa dansi. Alikuwa
ni mtu mwenye juhudi binafsi na upendo kwa wengine, lakini kazi ya Mungu haina
makosa,” alisema Mabela wa Msondo Ngoma.
Naye mmiliki wa Bendi ya Tabora Jazz,
Ibrahim Didi alisema Karenga ni miongoni mwa wanamuziki ambao wamejaaliwa
kipaji cha aina yake akiweza kuimba na kupiga gitaa kwa wakati mmoja.
"Nimepoteza jembe, isitoshe ni mtu
niliyetoka naye Tabora, pia hadi anafariki alikuwa yupo katika bendi hii ya Tabora
Jazz, imenima sana. Karenga alikuwa mtu wa watu," alisema Didi, kiongozi
wa zamani wa Yanga.
Mwingine aliyemzungumzia Karenga, ni Ally
Choki ambaye alikiri kuwa kwake alikuwa ni mwalimu wake wa kupiga vyombo hasa
gitaa akifanya naye kazi mwaka 1992.
"Alinifundisha mengi na alikuwa mwalimu
wangu katika tasnia hii..ya muziki, kwa kweli ametuachia pengo kwasababu ni
ambaye aliniongoza kaatika masuala mengi, nilikuwa namfuataga kwake Kariakoo
ili anifundishe na kweli alinifundisha,"alisema Choki.
Naye Sajenti mstaafu wa Bendi ya Polisi Jazz
ya jijini Dar es Salaam, Kassim Said Mapili, alisema Karenga Shem alikuwa ni
mpiganaji mkongwe katika tasnia ya muziki.
"Nilijuana naye wakati tulipokutana Tabora wakati yupo Lake
Tanganyika Jazz, alikuwa na uwezo mkubwa tofauti na vijana wa sasa hivi
wanashindwa kuimba bila ya kutumia 'playback' CD," alisema.
Shem Ibrahim Karenga, aliyezaliwa mwaka
1950, kitongoji cha Bangwe, Kigoma, alipata elimu ya msingi shule ya
Kimishionari ya Kihezya kuanzia mwaka 1957 hadi 1964.
Baada ya hapo, mwaka 1964 alijiunga na bendi
ya Lake Tanganyika Jazz ambayo maskani yake yalikuwa mjini Kigoma.
Tangu aingie Lake Tanganyika akiwa mwimbaji
na mcharazaji wa gitaa la besi, alikuwa na ujuzi wa kutengeneza gitaa kwa
kutumia vifaa vya kuokoteza.
Aidha katika miaka yake minne katika bendi
ya Lake Tanganyika Jazz, alijifunza vyombo vingine vya muziki kama Drums, Kinanda, gitaa la Rithym na
la Solo’. Sisi sote ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea.
No comments:
Post a Comment