Mkuu wa
Huduma kwa Wateja wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Laibu Leonard(kushoto)
akikabidhi msaada wa vyakula mbalimbali Muuguzi Mkuu wa Taasisi ya Saratani
Ocean Road, Mary Haule kwa ajili ya kuwafariji wagonjwa waliolazwa katika hospitalini
hiyo. Wa pili kushoto ni Meneja
Mauzo, Benjamin Bizere. (Picha na Francis Dande)
Mkuu wa
Huduma kwa Wateja wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Laibu Leonard (kushoto)
akikabidhi msaada wa vyakula mbalimbali Muuguzi Mkuu wa Taasisi ya Saratani
Ocean Road, Mary Haule kwa ajili ya kuwafariji wagonjwa waliolazwa hospitalini
hapo.Wa pili kushoto ni Meneja
Mauzo, Benjamin Bizere.
Muuguzi Mkuu wa Taasisi ya Saratani
Ocean Road, Mary Haule akipokea msaada wa vitu mbalimbali vilivyotolewa kwa ajili ya wagonjwa wa waliolazwa katika Taasisi ya Saratani jijini Dar es Salaam kulia ni Meneja
Mauzo, Benjamin Bizere.
Mkuu wa
Huduma kwa Wateja wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Laibu Leonardakizungumza na waandishi wa habari.
Muuguzi Mkuu wa Taasisi ya Saratani
Ocean Road, Mary Haule akizungumza na waandishi wa habari.
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
WAGONJWA wa saratani waliolazwa katika hospitali ya Ocean
Road wamepata msaada wa vyakula kwa ajili ya sherehekea Siku Kuu ya Krismas
inayotarajiwa kuadhimishwa kesho.
Msaada huo wenye tamani ya sh milioni tatu umetolewa na
Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL).
Akizungumza na wandishi wa habari wakati akikabidhi msaada
huo jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Huduma kwa Wateja, Laibu Leonard, alisema
msaada huo ni sehemu ya kurudisha faida kwa wateja wao.
Alitaja msaada huo kuwa ni unga, majisafi, mchele na mwingine
ambao utaweza kuwafariji, hususan katika kipindi hiki cha siku kuu hiyo.
“Hawa ni teja wetu ambao pia tunatarajia kuwafikishia
huduma za afya mtaandao katika kipindi cha miezi mitatu, ambao utawasidia
madaktari nchini kuwasiliana na wale wanje katika majidiliano yanayohusu
matibabu ya wagojwa bila kupata gharama
za kuwapeleka nje,”alisema Laibu.
Naye Muguuzi Mkuu wa Hospitali hiyo, Mary Haule, alisema
msaada huo umekuja katika kipindi muwafaka kwani kuna wagonjwa ambao wako
hospitalini hapo hawana ndugu, utawasaidia.
“Tunaishuru TTCL kwa Msaada huu, tunawaomba wadau wengine
watakaoguswa waige mfano huu,”alisema Mary.
No comments:
Post a Comment