HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 12, 2015

KILELE CHA MAADHIMISHO YA MIAKA 51 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

 Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiwapungia Mkono wananchi wakati alipowasili katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja katika kilele cha Sherehe za miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yaliyofanyika leo, (Picha na Ikulu)
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akikagua gwaride la vikosi vya ulinzi na usalama leo wakati wa  Sherehe za miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar akifuatana na Paredi Kamanda Luteni kanali Mohamed Khamis Adam  katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
Wananchi mbali mbali waliohudhuria katika sherehe za kilele cha miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar wakimasikiliza Rais wa Zanzibar.
 Wafanyakazi wa Ofisi ya rais Tawala za Mikoa na Idara maalum za SMZ wakipita mbele ya jukwaa kwa maandamano wakati wa sherehe za Kuadhimisha miaka 51 ya mapinduzi ya Zanzinar akiwa mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein.
Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakipita mbeke ya Mgeni Rasmi  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein kwa Mwendo wa Pole pole.
 Askari wa Kikosi cha Mafunzo SMZ  wakipita mbeke ya Mgeni Rasmi  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kwa Mwendo wa Pole pole katika sherehe za kuadhimisha miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar katika Uwanja wa Amaan.
Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kikosi cha Bendera wakitoa salamu ya Gwaride la mwendo wa haraka kwa  Mgeni Rasmi  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein  katika sherehe za kuadhimisha miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 Askari wa Jeshi la Polisi  Tanzania Kikosi cha FFU  wakitoa salamu ya Gwaride la mwendo wa haraka kwa  Mgeni Rasmi  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  katika sherehe za kuadhimisha miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 Askari wa Jeshi la wanamaji Zanzibar Kikosi  cha KMKM  wakitoa salamu ya Gwaride la mwendo wa haraka kwa  Mgeni Rasmi  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  katika sherehe za kuadhimisha miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 Askari wa Jeshi la kujenga Uchumi  Zanzibar (JKU) wakitoa salamu ya Gwaride la mwendo wa haraka kwa  Mgeni Rasmi.
Wasanii wa kutoka Gairo Mkoa wa Morogoro wakitoa burudani kwa ngoma ya Mtunya wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hotuba yake wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya sherehe za miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika leo katikauwanja wa Amaan Mjini Unguja.

No comments:

Post a Comment

Pages