Meneja wa Msamaha wa Mamlaka ya Kodi na Mapato Tanzania (TRA), Kyabukoba Mutabingwa (kulia), Mkurugenzi wa fedha Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Julius Angello pamoja na Mwanasheria Mwandamizi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Steven Urassa wakiingia katika chumba cha mahakama.
Mkurugenzi wa fedha Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Julius Angello akiwa chini ya ulinzi wa askari Polisi.
Mkurugenzi wa fedha Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Julius Angello akijifunika na suti yake kuficha sura yake wakati alipofika mahakamani.
Mkurugenzi wa fedha Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Julius Angello akijifunika na suti yake kuficha sura yake wakati alipofika mahakamani.
Watuhumiwa wakiwa chini ya ulinzi.
Mkurugenzi wa Fedha wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Julius Angello anadaiwa kupokea zaidi ya bilioni 1 kupitia akaunti namba 00120102646201 zikiwa ni sehemu ya fedha za Akaunti ya Tegeta Escrow.

Mkurugenzi wa Fedha wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Julius Angello akitoka mahakamani.

Mwanasheria Mwandamizi wa (Tanesco), Steven Urassa anakabiliwa na shitaka moja la kupokea zaidi ya sh. milioni mia moja kupitia namba 00120102658101 zikiwa sehemu ya Akaunti ya Tegeta Esrcow.
Na Mwandishi Wetu
VIGOGO wengine
watatu wamepanisha kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu wakikabilia
na mashitaka ya kujipatia fedha kwa njia rushwa kutoka kwenye Akaunti ya Tegeta
Escrow.
Vigogo waliopandishwa kizimbani leo katika mahakama hiyo ni Meneja wa Mamlaka ya Kodi Tanzania (TRA),
Kyabukoba Mutabingwa, Mkurugenzi wa fedha Benki Kuu ya Tanzania (BOT),
Julius Angello pamoja na Mwanasheria Mwandamizi wa Shirika la Umeme
Tanzania (Tanesco),Steven Urassa.
Mshitakiwa wa
kwanza katika sakata hilo, ambaye ni Mkurugenzi wa BoT, Angello alisomewa shitaka
lake na Wakili wa Serikali Leornda Swai akishirikiana na Max Ari mbele ya
Hakimu Mkazi Devotha Kisoka, huku upande wa utetezi ukiwakilishwa na Wakili
Jamuhuri Jonson.
Wakili Swai
alieleza kwamba mshitakiwa anakabiliwa na shitaka moja la kula rushwa Februari
6, 2014 katika benki ya Mkombozi wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, ambapo
alijipatia kiasi cha fedha zaidi ya bilioni 1 kupitia namba 00120102646201
zikiwa ni sehemu ya fedha za Akaunti ya Tegeta Escrow.
Alieleza
kwamba, mshitakiwa alijipatia fedhab hizo ikiwa ni tuzo kwa kusaidia malipo
yaliyofanyika kwenye Akaunti hiyo ya Tegeta baada ya kuwepo kwa makubaliano
baina na Kampuni ya IPTL, ikiwa kinyume na matakwa ya mwajiri wake.
Swai alieleza
kwamba upelelezi wa shauri hilo umekamilika, pia shitaka hilo halihitaji kibali
kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP).Pia aliiomba mahakama izuie matumizi
ya fedha hizo kutokana na fedha hizo zina kesi mhakamani hapo.
Hata hivyo
upande wa utetezi kupitia wakili wake Jonson ulimuomba hakimu atoe dhamana kulingana
na shitaka lenywe kwani mshitakiwa bado ni Mkurugenzi, pia kosa hilo
alikugundulika kwa siku moja.
Baada ya
kueleza hayo, Hakimu Kisoka alimuuliza mshitakiwa kuhusu shitaka hilo, lakini
mshitakiwa alikana mashitaka.
Hata hivyo alitoa masharti ya dhamana kwa
mshitakiwa huyo kutoa kiasi cha Sh milioni 80 taslimu au hati yenye thamani ya
fedha hizo, pamoja na wadhamini wawili ambao wanatakiwa kuwa na bondi ya
Milioni 50 kwa kila mmoja.
Hakimu Kisoka
alisema kwamba kwa kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na mtuhumiwa
kashindwa kutekeleza masharti ya dhamana anarudishwa rumande hadi Januari 27,
mwaka huu kwa ajili ya kukamilisha dhmana yake na usikilizwaji wa awali.
Pia mshitakiwa
wa pili kupandishwa kizimbani ni Mwanasheria Mwandamizi wa (Tanesco), Urassa
mbele ya Hakimu Mkazi Janeth Kaluyenda, ambapo upande wa Jamhuri uliwakilishwa
na wakili Swai, huku upande wa utetezi ukiwakilishwa na Jopo la Mawakili watatu
likiongozwa na Jamhuri Jonson, Francis Kugesha na Peter Kibatala.
Wakili Swai
alieleza kwamba, mshitakiwa anakabiliwa na shitaka moja la kupokea rushwa mnamo
Februari 14, mwaka jana katika Benki ya
Mkombozi Tawi la St. Joseph lililopo Ilala, ambapo kiasi hicho alichopokea ni
zaidi ya milioni mia moja kupitia namba 00120102658101 zikiwa sehemu ya Akaunti
ya Tegeta Esrcow ambazo alizipokea kutoka kwa Rugemalira.
Alidai kwamba
Urassa alizipokea fedha hizo ikiowa kama tuzo ya kuiwakirisha Tanesco kama
Shirika la uzarishaji umeme nchini mbele ya Mahakama ikiwa kinyume na matakwa
ya mwajiri wake.Swai aliongeza kwamba upelelezi wa shauri hiolo umekamilika,
pia anaiomba Mahakama izuie matumizi ya fedha hizo.
Baada ya
kusomewa mashitaka yake, Hakimu Kaluyenda alimuuliza mshitakiwa kama
anakubaliana na kosa hilo, lakini alikanusha.
Ili kupata
dhamana Hakimu Kaluyenda alimtaka mshitakiwa alipe fedha taslimu za Milioni 81
au hati yenye thamani ya fedha hizo, pamoja nawadhamini wawili, mmoja awe
mtumishi wa umma, pia wawe na vitambulisho pamoja na barua za ofisi
wanazofanyia kazi.
Baada ya
mshitakiwa kukamilisha baadhi ya vipengele vya dhamana, Hakimu Kaluyenda
alimuachia kwa dhmana mshitakiwa huyo, pamoja na kuahirisha kesi hiyo hadi
Februari 11, mwaka huu kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali.
Hata hivyo
mtuhumiwa wa tatu katika sakata hilo, ambaye ni Meneja wa Msamaha wa (TRA),
Mutabingwa alisomewa mashitaka yake na wakili Swai mbele ya Hakimu Kaluyenda.
Wakili Swai
alidai kwamba mshitakiwa anakabiliwa na makosa manne ya kutoa na kupokea
rushwa, ambapo kosa la kwanza la kupokea rushwa alilifanya Januari 17, 2014
katika Benki ya Mkombozi, kiasi cha zaidi ya Bilioni moja kupitia namba za
akaunti 0011020613801 zikiwa ni sehemu ya Akaunti ya Tegeta Esrcow kutoka kwa
Rugemalira.
Alieleza kwamba
mshitakiwa alizipokea fedha hizo ikiwa ni tuzo ya kuiwakilisha TRA pamoja na
Kampuni ya VIP ikiwa kinyume na matakwa ya mwajiri wake.
Shitaka la pili
linalomkabili Mutabingwa, inadaiwa kwamba Julai 15, mwaka jana kupitia Benki
hiyo ya Mkombozi alipokea rushwa ya zaidi milioni mia moja kupitia akaunti
namba ya benki 00110202613801 zikiwa sehemu ya Akaunti ya Tegeta ambazo
alizipokea kutoka kwa Rugemalira zikiwa kama tuzo ya kuiwakilisha TRA na
Kampuni ya VIP.
Pia shitaka la
tatu, inadai kwamba Agosti 26, 2014 kupitia benki hiyo hiyo, Mutabingwa alipokea
tena rushwa ya zaidi milioni mia moja kupitia Akaunti hiyo hiyo ya benki zikiwa
sehemu ya Akaunti ya Tegeta Esrow kutoka kwa Rugemalirab kama muwakilishi wa
TRA na Kampuni ya VIP.
Hata hivyo
katika shitaka la nne, Swai alieleza kwamba Novemba 14, 2014 kupitia Benki hiyo
hiyo ya Mkombozi iliyopo Ilala mshitakiwa alipokea zaidi ya Milioni mia moja
kupitia namba zile zile za akaunti yake kutoka kwa Rugemalira ikiwa kama tuzo
ya kuiwakilisha TRA na Kampuni ya VIP.
Baada ya kusoma
mashitaka hayo, Swai aliiomba Mahakama izuie matumizi ya fedha hizo hadi keszi
hiyo itakapoisha, pia sheria izingatiwe katika utoaji wa dhamana.
Hata hivyo Hakimu
Kaluyenda alimuuliza mshitakiwa kama anakubaliana na mashitaka hayo, lakini
alikanusha.Pia mshitakiwa alitakiwa kutoa fedha taslimu Bilioni 1, pamoja na
wadhamini watatu, wawili wakiwa watumishi wa umma pamoja na bondi ya Sh.milioni
340 kwa kila mmoja.
Baada ya kutoa
masharti hayo, Hakimu Kaluyenda aliahirisha kesi hiyop hadi Januari 29, mwaka
huu kutokana na mtuhumiwa kushindwa kukamilisha masharti ya dhamana na
mshitakiwa huyo alirudishwa rumande.

ni kwa neema tu unapewa nafasi ya kuwatumikia wenzako unajinufaisha wakati mahospitali hakuna dawa Mungu anawapigania watu wake mafisadi wanavuna walichopanda!
ReplyDelete