HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 06, 2015

Aga Khan kuisaidia Hospitali ya Temeke

Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema (katikati) akiongozana na viongozi wa hospitali ya Agakhan jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake leo katika hospitali hiyo.

NA MWANDISHI WETU 


HOSPITALI  ya Aga Khan  iliyopo  jijini Dar es salaam imesema itashirikiana na  hospitali ya Temeke iliyopo wilaya ya Temeke  kwa ajili ya kuhakikisha afya ya mama na mtoto inaboreshwa.


Hayo yalibainishwa na  Mkuu wa Wilaya ya Temeke,  Sophia Mjema  wakati ya ziara yake hospitalini hapo kujionea huduma  zitolewazo  na hospitali hiyo kwa kutumia vifaa vya kisasa.


Mjema alisema kupitia ushirikiano huo  Temeke hospitali itapata  fursa ya kupeleka wagonjwa wake Agha Khan hasa akina mama na watoto kufanyiwa vipimo vya afya na matibabu bure .


Aidha alisema mbali ya huduma hizo pia watalaamu wa Agha Khan  watawasaidia wa Temeke katika kuwapa mafunzo ya namna ya kutumia  vifaatiba vya kisasa hivyo kubadilisha na ujuzi.


Katika Ziara hiyo  Mjema aliwataka watanzania  kuacha kwenda kutibiwa nje ya nchi  kwa kuwa hivi sasa kuna hospitali zinazotoa huduma zote ambazo ziliwalazimu watu kwenda nje kutibiwa na aliwashauri watumie hospitali hiyo ambayo ina wataalam wa kutosha hususan kwa magonjwa yaliyoshindikana  sambamba na  vifaatiba vya kisasa.
  
Pamoja na mambo mengne, Mjema alitoa  shukrani za dhati kwa uongozi  wa Aga Khan  na kuwataka waendelee na moyo huo ili kutimiza malengo ya milenia katika sekta ya afya.

Kwa upande wake  Dk. Jaffer Dharsee wa hospitali ya Aga Khan alisema katika kudumisha ushirikiano  itatoa mashine ya CT Scan  pamoja na wataalam kwaajili ya hospitali ya Temeke ili  kuwarahisishia wakazi wa Wilaya hiyo .

Naye  Bertysheba ambaye ni mgonjawa aliyekwenda kupata huduma ya Mionzi  ya kansa hospitalini hapoa alisifu huduma  zitolewazo na Agha Khan  sambamba  na kuwatoa hofu wagonjwa wa kansa kutoogopa  kutibiwa kwa njia ya mionzi kwani ndiyo inayompa ahueni na anatumia kwa mwaka wa tatu sasa.

No comments:

Post a Comment

Pages