HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 15, 2015

BABA MZAZI WA MSANII DULLY SYKES AFARIKI DUNIA

BABA mzazi wa msanii mkongwe wa muziki nchini, Dully Sykes, Ebby Sykes amefariki dunia leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa mtoto wake wa kike aitwaye Raya Sykes amethibitisha taarifa hizo kwenye mtandao wa Instagram.

Raya katika ukurasa wake huo aliandika ‘Mungu akulaze mahala pema peponi baba angu mimi nilikupenda lakini Mungu alikupenda zaidi…nasikitika nipo mbali sitaweza kukuzika. Ulikuwa ni mtu mwenye upendo na kila mtu alikupenda, nakupenda sana baba angu RIP dady nitakukumbuka milele daima’.


Sykes alikuwa muimbaji na mpiga gitaa mashuhuri na ndiye anayedaiwa kumfundisha mambo mengi ya muziki mwanae.
Sykes alizaliwa February 24, 1952 ambapo tarehe hiyo mwaka huu alikuwa anatimiza miaka 63.

Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.
Bwana ametoa na bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe….

No comments:

Post a Comment

Pages