HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 05, 2015

Barcalys yazindua huduma za kuweka fedha kwenye mashine za ATMs

Add caption
Na Mwandishi Wetu

Benki ya Barclays Tanzania imethibitishia umma wa watanzania ukuaji wake wa kasi wa teknolojia kwa kuzindua huduma mpya na ya kisasa ya kuweka pesa kwenye mashine zake za ATMs nchini.
 
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam katika uzinduzi rasmi wa huduma hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa, Uchuuzaji na Mikakati wa  Benki hiyo, Bw Musa Kitoi alisema mashine hizo za kisasa za i-ATMs zimetengenezwa kwa teknolojia ya juu na zina sifa ya kipekee.

Alisema kwamba huduma mbalimbali kama kuweka na kutoa fedha taslimu na hundi sasa zinaweza kufanyika kupitia mashine hizo mpya na kurahisisha huduma za kibenki kwa wateja wao.

Aliongeza kwamba benki ya Barclays itaendelea kutoa huduma mbalimbali kwa wateja wake kwa ufanisi wa hali ya juu ikizingatia uhakiki wa huduma bora kwa wateja wake na kurahisisha maisha yao kwa ujumla.

“Barclays tunawajali wateja wetu na siku zote tunanuia kuwapa huduma za hali ya juu kufuatana na matakwa yao, pia bidhaa na huduma zetu hupangwa kufuatana na mahitaji ya wateja wetu,”
“Tunapenda kuwathibitishia kwamba tuko katika kiwango cha juu sana kiteknolojia katika soko na baadhi ya huduma zetu za kiteknolojia ya juu kama mfumo wa kutoa na kuchukua fedha bila kujaza fomu, utumaji wa fedha kwenye mashine, benki kwa njia ya simu na mwaka jana tumezindua service guarantee ikimaanisha uhakiki wa huduma na kutimiza ahadi na kuwapa wateja huduma bora na za uhakika,” alisema.

Aliongeza kupitia mfumo wao wa kidigitali wateja wao wanawezeshwa kujihudumia ili kujipatia muda wa kutosha kufanya shughuli zao bila kupoteza muda wao mwingi kukaa benki.
Bw Kitoi alisema benki ya Barclays itaendelea kuongoza katika soko kwa kutoa huduma bora na makini kwa kutumia teknolojia ya hali ya juu.

Kwa upande wake, Meneja Miradi na Mikakati wa Benki hiyo, Bi Jane Mbwilo alisema kwamba huduma hiyo ni masaa 24 na mteja anaweza kuweka kiasi chochote kwenye mashine hizo za ATM hapa nchini.

Alifafanua kwamba kwa sasa mashine zipo 24 lakini wapo katika mkakati w mwisho kuongeza mashine hadi kufika 30 katika maeneo kadhaa ya jijini la Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Pages