Mke wa Rais wa
Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Bibi. Daniela Schadt (mwenye nguo nyekundu) akisalimiana na
Mkurugenzi wa DSW Tanzania Bw. Peter Owaga mara baada ya kuwasili katika ofisi
za Shirika hilo zilizopo Tengeru jijini Arusha alipoenda kuzindua mradi wa
BEYOND 2015 hivi karibuni.
Mke wa Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya
Ujerumani Bibi. Daniela Schadt (mwenye
nguo nyekundu) akisikiliza maelezo mafupi kuhusu Shirika lisilo la Kiserikali
la DSW Tanzania kutoka kwa Mkurugenzi wa shirika hilo Bw. Peter Owaga mara
baada ya kuwasili katika ofisi za Shirika hilo zilizopo Tengeru jijini Arusha
juzi.Wa mwisho kushoto ni Mkuwa Wialaya ya Arumeru Mhe. Nyirembe Munasa
Mkurugenzi wa DSW
Tanzania Bw. Peter Owaga akizungumza jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi
wa BEYOND 2015 juzi jijini Arusha. Kutoka kushoto ni Mke wa Rais wa Shirikisho
la Ujerumani Bibi. Daniela Schadt, Mke wa Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania
Bibi. Wenday Marshall – Kochanke na Mratibu wa Programu za Vijana kutoka Wizara
ya Afya, na Ustawi wa Jamii Dkt. Elizabeth Mapella. BEYOND 2015 ni mradi
uliolenga kuongeza hamasa na ushawishi kwa wadau wa maendeleo kutoa kipaumbele
kwa vijana husasni katika Elimu, Afya ya uzazi na Ajira.
Baadhi ya washiriki wa
hafla ya uzinduzi wa mradi wa BEYOND 2015 wakimsikiliza Mkurugenzi wa DSW
Tanzania Bw. Peter Owaga (hayupo pichani).
Mke wa Rais wa
Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Bibi. Daniela Schadt(mwenye nguo nyekundu)
akisikiliza maelezo kuhusu mradi wa BEYOND 2015 kutoka kwa Mratibu wa mradi huo
Bi. Esther Mwanjesa (kushoto) kabla ya kuzindua rasmi mradi huo juzi jijini
Arusha. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa DSW Tanzania Bw. Peter Owaga na
kushoto kwa Mke wa Rais wa Ujerumani ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Nyirembe
Munasa.
Mke wa Rais wa
Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Bibi. Daniela Schadt akifuarahi mara baada
ya kukata utepe na kuzindua rasmi mradi wa BEYOND 2015, juzi jijini
Arusha.Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa DSW Tanzania ambao ndiyo watekelezaji wa
mradi huu Bw. Peter Owaga. Wengine ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Nyirembe
Munasa (nyuma ya Mke wa Rais wa Ujerumani) na Mratibu wa Mradi huo Bi. Ester
Mwanjesa aliyeshika kitabu.
Mke wa Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya
Ujerumani Bibi. Daniela Schadt akiteta jambo na Mkurugenzia wa DSW
Tanzania(katikati) pamoja na Mratibu wa Mradi wa BEYOND 2015 Bi. Esther
Mwanjesa mara baada ya kuzindua mradi huo juzi jijini Arusha.
Mke wa Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya
Ujerumani Bibi. Daniela Schadt akipokea zawadi ya Kimasai kutoka kwa Mwanamke
mjasiriamali Bibi.Salome Samwel wakati alipotembelea maonyesho ya biaadha zao
katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa mradi wa BEYOND 2015, juzi jijini Arusha.
Mke wa Rais wa
Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Bibi. Daniela Schadt akivaa heleni alizopewa
kama zawadi kutoka kwa Mwanamke wa mjasiriamali Bibi.Salome Samwel wakati
alipotembelea maonyesho ya biadhaa zao yaliyokuwa katika hafla ya uzinduzi wa
mradi wa BEYOND 2015, juzi jijini Arusha.
Mke wa Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya
Ujerumani Bibi. Daniela Schadt na
Mwanamke mjasiriamali mwenye asili ya Kimasai Bibi.Salome Samwel wakiwa katika
nyuso za furaha juzi jijini Arusha wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa
BEYOND 2015 unaoratibiwa na kutekelezwa na DSW Tanzania.
Mke wa Rais wa
Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Bibi. Daniela Schadt akiangalia zawadi ya michoro ya kitamaduni aliyopewa na
Shirika la DSW Tanzania wakati wa hafla uzinduzi wa mradi wa BEYOND 2015 juzi jijini Arusha.
Aliyemshikia zawadihiyo ni Mkurugenzi wa DSW Tanzania Bw. Peter Owaga na Afisa
Miradi wa DSW Tanzania Bi. Diana Shuma
(mwenye shati jeupe).
PIX8: : Mke wa Rais wa
Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Bibi. Daniela Schadt (katikati) akiwa katika
picha ya pamoja na wafanyakazi wa Shirika la DSW Tanzania wakati wa hafla ya
uzinduzi wa mradi wa mradi wa BEYOND 2015, juzi jijini Arusha.Waliokaa kutoka
kushoto ni Mke wa Balozi wa Ujerumani hapa nchini Bibi. Wenday Marshall –
Kochanke, Mkuu wa Wialaya ya Arumeru Mhe. Nyirembe Munasa, Mkurugenzi wa DSW
Tanzania Bw. Peter Owaga na Mratibu wa Programu za Vijana kutoka Wizara ya Afya
na Ustawi wa Jamii Dkt. Elizabeth Mapella. Na
Mpiga Picha Wetu, Arusha
No comments:
Post a Comment