TIMU ya Red Arrows FC ya Zambia, inatarajiwa kuwasili jijini
Dar es salaam, Tanzania Jumatatu ya wiki ijayo, kwa ajili ya kuweka kambi ya
mafunzo ya wiki moja kujindaa na msimu mpya wa Ligi Kuu ya Zambia 2015.
Uongozi wa klabu hiyo chini ya Mwenyekiti wake Kanali
Nolacso Chilando, ulitua jana Makao Makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),
sambamba na Ofisa Habari wa Red Arrow, Luteni Kanali, Melody Siisii.
Kwa mujibu wa taarifa ya TFF kwa vyombo vya habari, Chilando
na Siisii, waliambatana na Alex Chila, ambaye ni Ofisa Ubalozi wa Zambia nchini
Tanzania kujitambulisha uwepo wao nchini kuelekea wiki moja ya maandalizi.
Wakiongea na Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mweisgwa,
viongozi wa timu hiyo wamesema maandalizi ya kambi yameshakamilika na kikubwa
walikua wanaiomba TFF kutambua uwepo wao na kuwasaidia kupata viwanja vya
kufanyia mazoezi.
Naye Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa alisema wameyapokea maombi
hayo ya Red Arrows FC na kuwakaribisha nchini kwa ajili ya kambi yao na kusema
ujio wao utafungua milango kwa vilabu vingine pia kuja kuweka kambi nchini. Red
Arrows inayomilikiwa na Jeshi la Anga la Zambia, ikiwa nchini kwa mafunzo,
inatarajia kucheza mchezo mmoja wa kirafiki na imeliomba TFF kuwatafutia timu
moja ya kucheza nayo.
No comments:
Post a Comment