HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 08, 2015

UTT-AMIS YATOA ELIMU YA UWEKEZAJI KWENYE MASOKO YA FEDHA KWA WABUNGE

 Ofisa Masoko wa Kampuni ya UTT, Bi. Kilave (kulia) akiwa na Ofisa Mkuu wa Kampuni ya Maendeleo ya Miundombinu ya UTT-PID, Shakiru Abdulkarim wakitoa elimu ya Uwekezaji kwenye Masoko ya Fedha kwa Wabunge na Watumishi wa ofisi ya Bunge wakati wa maonyesho ya kazi zinazofanywa na makampuni ya UTT na kufanyika katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
Maofisa Mafunzo kutoka UTT-Microfinance, Hilda Lyimo na Pauline, wakitoa maelezo kwa baadhi ya wabunge waliotembelea banda lao kuhusu Mikopo wanayotoa, pia wabunge walipata elimu fursa ya kujua shughuli mbalimbali zinazofanywa na makampuni ya UTT ambayo ni Maendeleo ya Miundombinu, Uwekezaji kwenye Masoko ya Fedha na Microfinance.

Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa UTT-AMIS, Daudi Mbaga (kulia) akitoa maelezo kuhusu shughuli za Makampuni ya UTT kwa baadhi ya wabunge waliotembelea banda lao.
Maofisa wa UTT Microfinance (kulia), wakitoa elimu kwa baadhi ya wabunge kuhusu shughuli za Makampuni ya UTT ambayo ni Maendeleo ya Miundombinu, Uwekezaji kwenye Masoko ya Fedha na Microfinance.

No comments:

Post a Comment

Pages