Mwandaaji wa Kipindi cha Walinde Watoto, Kimela Bila akizungumza katika warsha ya siku tatu inayohusu nafasi ya vyombo vya habari
katika kuzuia ukatili dhidi ya watoto iliyoandaliwa na Wizara
ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kwa ushirikiano na UNICEF.
Ofisa Maendeleo ya Jamii mkoa wa Kilimanjaro, Paul Shayo, akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya waandishi wa habari inayohusu nafasi ya vyombo vya habari katika kuzuia ukatili dhidi ya watoto iliyoandaliwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kwa ushirikiano na UNICE.
Baadhi ya washiriki wa Warsha wakifuatilia kwa makini.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada kwa makini
Baadhi ya washiriki wakiuliza maswali katika warsha hiyo
Mtangazaji wa kipindi cha Walinde Watoto kutoka kampuni ya True Vision Production, Janeth Sosthenes Mwenda, akisoma matarajio ya washiriki ya Warsha
Wizara
ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kwa ushirikiano na UNICEF
wameandaa warsha ya siku tatu inayohusu nafasi ya vyombo vya habari
katika kuzuia ukatili dhidi ya watoto nchini Tanzania.
Ofisa Maendeleo ya Jamii mkoa wa Kilimanjaro, Paul Shayo, akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya waandishi wa habari inayohusu nafasi ya vyombo vya habari katika kuzuia ukatili dhidi ya watoto iliyoandaliwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kwa ushirikiano na UNICE.
Baadhi ya washiriki wa Warsha wakifuatilia kwa makini.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada kwa makini
Baadhi ya washiriki wakiuliza maswali katika warsha hiyo
Mtangazaji wa kipindi cha Walinde Watoto kutoka kampuni ya True Vision Production, Janeth Sosthenes Mwenda, akisoma matarajio ya washiriki ya Warsha
Waandaaji wa kipindi cha Walinde Watoto kutoka kampuni ya True Vision Production wakiendelea na maandalizi ya Warsha. Kutoka Kushoto, Kimela Billa, David Sevuri na Bill Marwa.
Na Mwandishi Wetu
Warsha hiyo inayofanyika mjini Moshi inashirikisha wawakilishi kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Wawakilishi kutoka Mkoa wa Kilimanjaro, Wawakilishi kutoka wilaya za Hai na Moshi Manispaa, wawakilishi kutoka UNICEF pamoja na wawakilishi wa redio 14 zinazorusha kipindi cha Walinde Watoto.
Wengine ni wawakilishi kutoka Baraza la Habari Tanzania, mwakilishi kutoka Csema pamoja na waandaaji wa kipindi cha Walinde Watoto kampuni ya True Vision Production.
Akifungua
warsha hiyo, Afisa Maendeleo ya Jamii wa Mkoa wa Kilimanjaro, Paul
Shayo alilishukuru shirika la Watoto Duniani (UNICEF) kwa kazi nzuri
ambazo wamekuwa wakizifanya kwa kushirikiana na Serikali katika
kuhakikisha kuwa Haki za Watoto zinatekelezwa hapa nchini.
Paul
alitaja aina za ukiukwaji wa haki za mtoto hapa nchini kuwa ni pamoja
na kuolewa katika umri mdogo, kutumikishwa katika mashamba na ukatili
dhidi ya watoto. Hata hivyo aliendelea kuzitaja athari mbalimbali
zinazotokana na ukiukwaji wa haki hizo kuwa ni pamoja na watoto kukatishwa
masomo na kukosa haki ya
kuendelezwa na kwamba ndoa za utotoni zina
madhara kiafya hasa wanapopata ujauzito na kujifungua katika umri
mdogo.
Paul
alimalizia kwa kutoa rai kwa washiriki wa warsha hiyo na kuwataka
wakawe chachu ya kuzuia ukatili dhidi ya watoto katika maeneo waliyotoka
na kushirikiana na wadau waliopo katika ngazi za vijijini, mikoani na
mijini kadri inavyowezekana ili kuwalinda watoto na kutokomeza ukatili
dhidi ya watoto.
Vipindi
vya Walinde Watoto vinarushwa na redio 14 ambazo ni Radio Jamii Kilosa,
Country FM, Boma Hai FM, Radio Quran, ZBC pamoja na Redio Kitulo.
Nyingine
ni TBC Taifa, Bomba FM, Faraja FM, Uplands FM, Ice Fm, Radio Maria,
Radio Kwizera na Zenj FM. Vipindi hivi vinapatikana pia katika tovuti
ya www.walindewatoto.org na kupitia www.facebook.com/ WalindeWatoto
No comments:
Post a Comment