CHAMA cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), kimemjia juu Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kikidai, Mauaji na
Maafa ya Wakulima na Wafugaji, Mbigili na Mabwegere, yametokana na Serikali kupitia
kwa Pinda, kutomsikiliza aliyekuwa Mwanasheria Mkuu, Jaji Fredrick Werema.
Akihojiwa na Tanzania
Daima Jumatano, Mwenyekiti wa Tawi la Chadema Mbigili, Maftaha Hamis, alisema, Chadema
kimejifunza kwa masikitiko, kuona Mauaji na Maafa ya Wakulima na Wafugaji, Mbigili
na Mabwegere, yametokana na Pinda, kutomsikliza Jaji Werema.
Ndani ya barua ya Werema
aliyomwandikia Pinda gazeti limefanikiwa kuona alisema, amebaini Uhalali wa
Kijiji kinachojiita ‘Mabwegere’ (Usajili Na. 32758 wa 8.12.198), una shaka kwa
sababu, kilipata Hati ya kumiliki Ardhi miaka 10 kabla ya kuanzishwa, Hati Na. MG/KJJ.522
ya Juni 16, 1999.
Hamis alidai, “Katika barua
ya AG Kumb. AGC/G.20/19/162 ya 1.8. 2014, siku chache kabla ya Maafa ya
kuchomwa Moto Nyumba 40, ikifuatiwa na Vifo vya wakulima wawili na Mfugaji
mmoja, Werema alimwandikia Pinda akisema, ‘Ninashauri hatua hizo zichukuliwe
haraka’”.
Ushauri wa Werema
ulitokana na barua ya Waziri Mkuu Kumb. PM/P/1/569/29 ya Mei 8, 2014 kwa aliyekuwa
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, na kunakiliwa kwa AG kwa lengo la
kujadiliwa, ambapo Werema na Bendera, walikutana mara Mbili kwenye Ofisi zao.
Kwenye uchambuzi wa Kesi
za Hukumu ya Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa kuhusu Mgogoro wa Ardhi kati ya
Kijiji cha Mabwegere na Vijiji Jirani, AG alitaja, “Mambo muhimu aliyogundua
juu ya hukumu hizo, zilisababisha damu za watu kumwagika na mali kupotea.
“(i)Mahakama haikutoa
uamuzi wowote kuhusu uhalali wa kuanzishwa kwa Kijiji cha Mabwegere; (ii)
Mahakama haikuilekeza Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa, kuipa hadhi ya Kijiji,
Kijiji cha Mabwegere, Jukumu hilo si lake;
“(iii) Mahakama iliamua
kwamba, Hati ya kumiliki Ardhi iliyotolewa kwa kinachoitwa Kijiji cha Mabwegere
ni Hati halali; na (iv) Mahakama iliamuru kwamba, haukutolewa ushahidi wa
kuthibitisha kwamba, Hamis Msabaa na wenzake 37, walivamia kijiji cha Mabwegere”.ilisema
sehemu hiyo ya barua ya AG kwa Pinda.
Aidha Werema alisema,
kumbukumbu zinatoa tafsiri kwamba, Kijiji cha Mabwegere kilimilikishwa Ardhi
miaka 10 kabla ya kuanzishwa kwake. Kisheria Kijiji au Mtu asiyekuwepo, hawezi
kumiliki Mali ikiwa ni pamoja na Ardhi; Hivyo Kijiji cha Mabwegere kumilikishwa
Ardhi kabla ya kuanzishwa kwake, kunatia shaka.
No comments:
Post a Comment