HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 20, 2015

MUSWADA BINAFSI WA KUANZISHWA BARAZA LA VIJANA LA TAIFA KUJADILIWA MACHI 31

HATIMAYE muswada binafsi wa kuanzishwa Baraza la Vijana la Taifa uliyowasilishwa bungeni Oktoba 31, 2013 na Mbunge wa Ubungo John, umepangwa kusomwa kwa mara ya pili na kujadiliwa Machi 31 mwaka huu katika Mkutano wa 19 wa Bunge linaloendelea mkoani Dododoma.
Mnyika, alisema Muswada huo ulisomwa kwa mara ya kwanza katika Mkutano wa 14 wa Bunge Disemba 21, 2013, umetokana maoni ya wadau yalikusanywa Oktoba 2014 na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii.
Akizungumza kwa njia ya simu mbunge huyo alisema kuwa pamoja na malengo mengine baraza hilo pia litawezesha vijana kuanzia kwenye vijiji, mitaa hadi taifa kuweza kuwa na vyombo vya kuwaunganisha vijana wa kike na wa kiume kwa ajili ya maendeleo yao na ya taifa.
Alisema Kujadiliwa kwa muswada huo ni hatua ya pekee katika historia ya harakati za vijana nchini kwa kuzingatia kuwa Sera ya zamani ya maendeleo ya vijana ya mwaka 1996 ilitamka kwamba kutaanzishwa Baraza la Vijana na suala hilo kurudiwa katika Sera mpya ya mwaka 2007.
“Natambua mchango wa vijana na taasisi zote za vijana mlioshiriki katika maandalizi ya muswada huu, unaitwa binafsi kwa sababu tu ndio neno linalopaswa kutumika kwa mujibu wa Kanuni za Bunge lakini ukweli ni kwamba huu ni muswada wenu; mimi ni mwakilishi,”alisema Mnyika.

Hata hivyo, alisema kuwa Serikali imekuwa ikikwepa kuhakikisha kwamba matakwa hayo ya sera tajwa yanatekelezwa kwa wakati pamoja na kuwa suala hilo linahusu mustakabali wa maendeleo ya vijana nchini.

Aidha, Baraza hilo litafuatilia pia kwa karibu utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya vijana ikiwemo kuhusu ajira, elimu na sekta zingine katika Halmashauri, Serikali kuu, katika vyombo mbalimbali vya maendeleo na wadau wa maendeleo.
Mnyika, alisema pia Muswada huo utawezeshwa kuanzishwa kwa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana na kulipa jukumu Baraza la Vijana kufuatilia kwa karibu utendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana; kuhakikisha kwamba fedha zinatengwa za kutosha na kufika kwa walengwa kuwawezesha vijana kujiajiri, kukuza vipaji vyao na kushughulikia maendeleo yao kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment

Pages