Mwenyekiti wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani), jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki kuhusiana na ujio wa mwimbaji nyota kutoka Afrika Kusini Thori Mahlangu (Obrigado). (Picha Francis Dande)
Msama akifafanua jambo.
Na Loveness Mboje
RAIA wa Afrika Kusini
ambaye ni Mwanamziki wa nyimbo za injili, Thori Mahlangu (Obrigado),
amethibitisha kuwa mmoja wa waimbaji wa kimataifa watakaotumbuiza katika
Tamasha Pasaka litakalofanyika Aprili 5.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha
hilo, Alex Msama alisema kuwa sambamba na mwimbaji huyo ataambatana na waimbaji
wengine 16 kutoka nchini humo huku Faustine Munishi maarufu kwa jina la Malebo na
Solomon Mukubwa kutoka nchini Kenya nao
watakuwepo.
Msama alisema kuwa viingilio vya tamasha hilo kwa watoto vitakuwa shs. 2,000 viti vya kawaida shs.5,000 VIP B, shs. 10000 VIP A shs. 20,000 kwa watu wakubwa na kuongeza kuwa mara baada
ya tamasha hilo, Aprili 12 itakuwa ni zamu ya wakazi wa jiji la Mwanza katika Uwanja wa CCM Kirumba.
Aidha kwa upande wa waimbaji wazawa Msama amesema kuwa mwimbaji Joshua Mlelwa ambaye alikuwa
mwimbaji wa Upendo Group naye atapamba tamasha hilo ambalo linasubiliwa kwa hamu kubwa na mashabiki.
Tamasha hilo linatimiza
miaka 15 tangu lianzishe
na linatarajiwa kihudhuriwa na watu mbalimbali kutoka
nchi za Kenya, Uganda,Rwanda, Afrika Kusini Uingereza na
wenyeji Tanzania.
No comments:
Post a Comment