HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 18, 2015

TTCL yakabidhi msaada wa chakula kwa wahanga wa mafuriko Kahama


Meneja wa TTCL mkoa wa Shinyanga Peter Kuguru akizungumza  wakati wa kukabidhi msaada wa chakula kwa wahanga wa mafuriko Kahama.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya (Kushoto) akipokea msaada kutoka kwa Meneja wa TTCL mkoa wa Shinyanga Peter Kuguru (Kulia)

Na Mwandishi Wetu
 
Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) yakabidhi msaada wa chakula kwa wahanga wa mafuriko Kahama. Msaada uliotolewa ni pamoja na mchele kilo 740, unga kilo 600, maharage kilo 300 na mafuta ya kupikia lita 260.


Msaada huo umekabidhiwa na Meneja wa TTCL mkoa wa Shinyanga Peter Kuguru kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Dkt. Kamugisha Kazaura.


Akizungumza baada ya kukabidhi msaada huo, Meneja wa TTCL Bw. Peter Kuguru alisema TTCL inawapa pole sana wahanga wa tukio hilo na kwamba TTCL imepokea kwa huzuni kubwa tukio hilo na kuwataka Watanzania kuwaombea waliopatwa na janga hilo wapate faraja na kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu waliopoteza maisha awapumzishe mahali pema peponi.


Naye Mkuu wa  Wilaya ya Kahama Mhe.Benson Mpesya akizungumza baada ya kupokea msaada huo, aliishukuru TTCL  kwa kuona umuhimu wa kuwafikia wahanga wa mvua hiyo na kuongeza kuwa TTCL wamekuwa na moyo wa huruma kwa wahanga hao huku akiahidi kuwa misaada inayotolewa na watu wenye mapenzi mema itatumika kwa wahanga wa tukio hilo na si vinginevyo na atakuwa mkali kwa hilo.

No comments:

Post a Comment

Pages