HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 19, 2015

Usalama wa kutosha Tamasha la Pasaka

Mjumbe wa Kamati ya maandalizi ya tamasha la Pasaka, Khamis Pembe, akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusu tamasha hilo litakalofanyika Aprili 5.  Kushoto ni Mwenyekiti wa tamasha hilo, Alex Msama. (Picha na Francis Dande).
 Mwenyekiti wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusu tamasha hilo litakalofanyika Aprili 5. Kushoto ni Mwenyekiti wa tamasha hilo, Alex Msama.

NA LOVENESS BERNARD

KAMATI ya Tamasha la Pasaka, imewahakikishia usalama wapenzi wa muziki wa Injili na Watanzania kwa jumla katika tamasha hilo litakalokata utepe Aprili 5 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mjumbe wa Kamati hiyo, Khamis Pembe, alisema tayari wamewasiliana na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna (CP), Suleiman Kova.

Alisema maandalizi ya Tamasha la Pasaka yamekamilika asilimia 90 na mwaka huu litakuwa la aina yake.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Alex Msama, alisema mwaka huu tamasha linaadhimisha miaka 15 tangu lianzishwe na wanatarajia kumwalika Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi kujumuika nao, kwani ndiye alikuwa mgeni rasmi wakati linaanzishwa.

Msama aliwataja waimbaji wengine watakaokuwepo katika tamasha hilo kuwa ni pamoja na John Lisu na Kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama huku wakiwa katika mazungumzo na mwimbaji nguli wa nyimbo za Injili, Rose Muhando, kutokana na maombi ya wapenzi wengi wa tamasha hilo.

No comments:

Post a Comment

Pages