MCHUNGAJI, Alphonce
Temba, wa Kanisa la Penuel Healing Ministry Dar es Salaam, amesema ataacha
Madhabahu kuwahubiri Waumini, na badala yake atakwenda kushirikiana na
Wanasiasa kuwaelimisha Wananchi ili Tanzania impate Rais mwenye Sifa, na atakayetatua
Ajali zinazomaliza Maisha ya Watu.
Akizungumza ITV katika
Kipindi cha Kumekucha asubuhi Aprili 27, mwaka huu, Temba alisema, Tatizo kubwa la
ajali zinazomaliza Watanzania nchini
zinatokana na Uzembe wa Viongozi, Ubovu na Uchache wa Miundo mbinu ya barabara
zetu na kudai, ataacha Madhabahu na kuungana na Wanasiasa, kuhakikisha
anapatikana Rais mwenye Sifa, atakayezua ajali.
Hata hivyo Mchungaji
Temba, alimshambulia Waziri wa Ujenzi John Pombe Magufuli akisema, ajali nyingi
zimetokea na watu wengi wamekufa kwa kumwaga damu, lakini hajasikika akitoa
tamko lolote na akamtuhumu kuwa, kuna Sheli za Mafuta na Gereji zimejengwa
barabarani (mfano Kibaha), lakini hachukui hatua.
Temba alidai, “Nadhani Magufuli
amechoka na anatakiwa kusaidiwa na Vijana wengine wasomi, ambao wana uwezo
mkubwa wa Teknologia mpya lakini wanakosa kazi. Ingawa wanasiasa wanasema Viongozi
wa dini tusiwaingilie, tupo kwa ajili ya
kuwakemea.
“Katika nchi za wenzetu
kuna barabara sita na magari yanakwenda mwendo wa kasi, lakini hakuna ajali! Kwetu
kuna ajali kwa sababu barabara ni moja, Malori yanaingia mjini badala ya
kuishia nje ya mji ili kupunguza msongamano”.
Mbali ya kumshambulia
Waziri Magufuli, pia Temba aliwaone Askari wa Usalama barabarani (Traffic) na
kuwavaa Watendaji wa Wakala wa Barabara
Tanzania (TANROAD)
akidai, Polisi sasa hivi wamefanywa kama TANROAD, walichobakiza ni kujenga kwa
sababu, siku hizi kila kitu ‘Traffic’.
Temba alishauri, Safari
za Mabasi kusafiri usiku, zierejeshwe kwa sababu zitapunguza msongamano wa
Magari, na kudai, Viongozi wa dini na Wananchi waheshimiwe, na kwamba, sasa
kazi yetu iwe ni kuwafukuza wafanyakazi wazembe, ili wasomi wasio na kazi
wachukue nafasi zao maendeleo ya nchi yaende.
No comments:
Post a Comment