HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 17, 2015

MSHINDI WA 'TUMA PESA NA SimBanking' AKABIDHIWA GARI

 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akimkabidhi akizungumza katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa shindano la ‘Tuma Pesa na SimBanking Shinda Passo’.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akimkabidhi mfano wa fuguo ya gari Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Mzumbe Jane Maganga ambaye alipokea kwa niaba ya mshindi wa kampeni ya ‘Tuma Pesa na SimBanking Shinda Passo’,  Bayinga Majeshi katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni mshindi wa Solar Pannel, Winnie Richard na Peter Fundi aliyejishindia simu ya mkononi.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akimkabidhi mfano wa fuguo ya gari Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Mzumbe Jane Maganga ambaye alipokea kwa niaba ya mshindi wa kampeni ya ‘Tuma Pesa na SimBanking Shinda Passo’,  Bayinga Majeshi katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni mshindi wa Solar Pannel, Winnie Richard na Peter Fundi aliyejishindia simu ya mkononi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akimkabidhi zawadi ya Sola Pannel, Winnie Richard baada ya kuibuka mshindi wa pili katika shindano la ‘Tuma Pesa na SimBanking Shinda Passo’.
 Mkurugenzi wa Masoko Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akizungumza katika hafla hiyo.
Yunis Nyanda akipokea zawadi yake.
 Peter Fundi akipokea zawadi yake.
 Lilian Mngulu akipokea zawadi yake.
Baadhi ya washindi wa shindano la ‘Tuma Pesa na SimBanking Shinda Passo’ wakipokea kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei mfano wa funguo ya gari kwa niaba ya mshindi wa kwanza wa shindano hilo, Bayinga Majeshi kutoka Morogoro ambaye alishindwa kuhudhuria hafla hiyo. Kulia ni Meneja wa benki hiyo tawi la Mzumbe, Jane Maganga.
 Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Mzumbe, Jane Maganga akijaribu kuwasha gari la mshindi.
 Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Mzumbe, Jane Maganga akionyesha furaha yake baada ya kujaribu gari la mshind.
 Baadhi ya washindi wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei pamoja na Mkurugenzi wa Masoko Huduma kwa Wateja, Tully Mwambapa na Meneja wa Tawi la Mzumbe, Jane Maganga wa pili kushoto.
 Baadhi ya Wakurugenzi wa benki ya CRDB pamoja na wageni waalikwa wakiwa katika hafla hiyo.
Picha ya pamoja.

Na Francis Dande

MWEKA Hazina wa Chuo Kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro, Bayinga Majeshi (40), ametangazwa mshindi wa gari jipya aina ya Toyota Passo, baada ya kuibuka mshindi wa kampeni ya ‘Tuma Pesa na SimBanking Shinda Passo’ inayoratibiwa na Benki ya CRDB.

Kampeni hiyo maalum ya Benki ya CRDB, inawapa nafasi wateja wakw kujisahindia zawadi mbalimbali, zikiwwmo simu za mkononi, kompyuta, Solar Pannel na sawadi kuu ambayo ni gari jipya la Toyota Passo, ambalo Majeshi ameshinda.

Majeshi aliekabidhiwa gari jana, anakuwa mshindi wa pili kujitwalia Toyota Passo, akifuata nyayo za mshindi wa kwanza Tumaini Mwakajwangwa, ambaye alijibebea gari hiyo katika droo ya mwezi uliopita wa kampeni hiyo.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi hizo, iliyofanyika katika Tawi la CRDB Kijitonyama, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dk. Charles Kimei, alisema lengo la kampeni huyo ni kushawishi wateja kuendelea kutumia njia mbadala za kutolea huduma.

“Faida za njia mbadala katika kutoa huduma ‘Altenative Banking Channels’ ni kuwapa wateja urahisi na kufurahia huduma zetu mahali popote walipo na kwa wakati wautakao bila ulazima wa kutembelea matawi yetu,” alisema Dk. Kimei.

Kwa upande wake mshindi huyo aliitaja siri ya kuweza kujinyakulia Toyota Passo kuwa ni kuhakikisha kila muamala unaotaka kuufanya katika akaunti yako, unaufanyia kupitia SimBanking, ambayo ni njia rahisi na bora zaidi.

“Mimi nimeshaacha kwenda kwenye tawi la CRDB pale Mzumbe ili kupata huduma, badala yake nimejijengea utaratibu wa kufanya kila kitu kupitia SimBanking. Nalipia maji, nanunua Luku, muda wa maongezi, na mengineyo kupitia SimBanking,” alisema Majeshi.

Washindi wengine wa mwezi huu na zawadi zao kwenye mabano ni pamoja na Winnie Samanya wa CRDB Mbezi Dar (Solar Pannel), Lilian Mngulu wa CRDB Azikiwe (Tablet), Peter Fundi wa CRDB Tanga (Simu) na Yunis Nyanda wa CRDB Tanga (Simu).

No comments:

Post a Comment

Pages