Na Bryceson Mathias, Kilosa,
Morogoro
MWENYEKITI wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tawi la Mbigiri Wilaya ya Kilosa, mkoani
Morogoro, Maftaha Hamisi Shabani, amekamatwa na Polisi Dumila, bila kuelezwa ana
Kosa gani.
Katibu wa Tawi hilo Mohamed Ami, amethibitisha Mwenyekiti wake, Shabani,
kukamatwa na Polisi akiwa Dumila, na kwamba, wengine waliokamatwa kabla yake ni
Pamoja na Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji hicho, Hemed Salum (CCM).
Ni kweli Mwenyekiti wa
Chadema Mbigiri (Shabani) amekamatwa na Polisi akiwa matembezini Dumila, na
wengine waliokamatwa naye ni Mtendaji wa Mbigiri, Jacb Mvungi, ambapo makosa
yao bado hayajawekwa wazi, isipokuwa dhamana yao.
Imedaiwa mapema siku
ya nyuma yake, Wafugaji wa Jamii ya
Kimasai waliingiza Makundi ya Ngombe kwenye Mashamba ya Wakulima katika Kijiji
cha Mbigiri, ambapo Wakulima wa Mbigiri walipoziswaga Ngombe hizo ili
kuilalamikia Polisi kwa uharibifu, kibao kimewageukia.
Imeelezwa baada ya
Wafugaji hao kukimbia na kuacha Ngombe, ghafla walitokea polisi na kuanza
kuwakamata Viongozi wa Kijiji cha hicho wakiwemo Mwenyekiti wa Serikali ya
Kijiji, (Salum na Mtendaji Mvungi), ambapo alifuatia Mwenyekiti wa Chadema
Shabani.
Habari zingine zinadai,
Viongozi na baadhi ya Wana Kijiji cha Mbigiri walipokwenda Polisi kutaka
kuwawekea Dhamana ndugu zao, badala ya kutoa Dhamana, Polisi walikuwa
wakiwakamata na kuwaweka ndani, jambo lililowafanya Wananchi kuogopa kwenda.
OCD wa Kituo cha Polisi
cha Dumila, Jafari Rashid Kiyoga, alipoulizwa juu ya tukio hilo, alikataa
kusema lolote akidai si Msemaji ila Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro, Leonard
Paul, ambapo hakupatikana kwa simu hadi tunakwenda mitamboni.
Wananchi na Viongozi wa
Mbigiri bila kujali itikadi zao, wamelilalamikia Jeshi la Polisi wakidai,
limekuwa Jeshi la Wafugaji wilani Kilosa na Mkoa, limekuwa na Upendeleo wa
upande mmoja, ambapo Wafugaji wakilisha Ngombe mazao yao, wakiambiwa
hawashughuliki, ila wanapochukua hatua za kuswaga Ngombe kama ushahidi ili
wawashitaki, nguvu kubwa ya Polisi inatumika kwao.
No comments:
Post a Comment