Waziri Kivuli wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Suzan Lyimo (Chadema) akifafanua
jambo jijini Dar es Salaam leo, kuhusu matatizo katika sekta ya elimu. Kushoto
ni Katibu wa Bawacha, Grace Tendega. (Picha na Francis Dande)
Na MwandishiWetu
WAZIRI kivuli wa
Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Suzan Lymo, amepinga kitendo cha serikali cha
kuwataka walimu waliofunga shule kutokana na uhaba wa chakula waende
wakajieleze kwa Mkuu wa Mkoa kutokana na hatua hiyo.
Suzan, alitoa
kauli hiyo baada ya serikali kudai kuwa tayari ilikuwa imekwishapeleka fedha
hivyo walimu hao hawakupaswa kufanya hivyo.
Akizungumza na
wandishi wa habari jijini Dar es Salaam ,
Waziri huyo kivuli, alisema jambo hilo
halishangazi kwa vile inaeleweka kuwa serikali legelege huzaa maamuzi mabovu
yasiyo na mantiki.
“Cha ajabu leo
hii watoto wanarudishwa nyumbani au kucheleweshwa kutofungua shule baada ya
likizo ya Pasaka, kwa kuwa wazabuni hajalipwa fedha zao na hivyo hawawe kununua
vyakula tena,”alisema Zuzan.
Alisema, hatua za
walimu kuwarudisha nyumbani wanafunzi, zilikuwa sahihi kwani kama
wangewaacha shuleni hapo huku kukiwa hakuna chakula ieleweke wazi kuwa
wanafunzi hao wangefanya vurugu ambazo zingeweza kuleta matatizo mengine.
“Nawapongeza
walimu wakuu kwa utaratibu huo swali ni je walimu wanajua kiasi cha fedha
wanachopaswa kupewa?
“Hii ni aibu
kubwa kwa serikali, kama mdau wa elimu imenisikitisha sana na ninatambua kuwa
baadhi ya wazabuni ni wazalendo na wengine hata wanakopa kwa ajili ya kulisha
wanafunzi hawa lakini wamefika ukomo,”alisema Suzan.
Suzan, alisema
kuwa mwezi wa tano ni wa mitihani ya kidato cha sita hivyo wanafunzi wanapaswa
kusoma kwa bidii bila bugudha ili waweze kufanya vizuri.
“Nashangaa baadala ya kufanya hivyo
wanavurugwa huku wenzao washule binafsi wakiendelea na masomo sasa kutokana na
wanafunzi hao kupoteza vipindi matokeo yake ni wanafunzi kufeli
mitihani,”alisema Suzan.
Hata hivyo,
alishangazwa kusikia kuwa hadi sasa ni asilimia 62 ya fedha za kulisha shule
zimetolewa wakati hii ni robo ya mwisho wa mwaka, ambapo ilitakiwa kufikia
kipindi hiki iwe ilipswa asilimia 75 zimekwisha lipwa.
No comments:
Post a Comment