HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 05, 2015

ABIRIA WALALAMIKIA OFISI YA MKUU WA MKOA WA MBEYA

NA KENNETH NGELESI,MBEYA

BAADHI ya abiria jiji Mbeya wamwtupia lawama Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas kwa kushindwa kufika katika kituo cha mabasi kwa lengo la kuwa julia hali abiri ambao wamekwama kwa siku ya pili kutokana na mgomo wa madereva.

Wakizungumza kabla ya mabasi kuanza safari kuekea mikoa mbalimbali, abaria hao walisema kuwa hapo kituo kuna watu wenye matatizo tofauti hivyo wanaitaji misaada mbalimbali lakini wanashangazwa tangu mgomo huo uanze juzi  viongozi wameshindwa kufika kituo hapo kuweza kuongea na abiria.

Neema Mabula amabaye alikuwa anasafiriki kutoa Chunya kuelekea jiji Dar-es-salaam,alisema ni jambo la ajabu sana kuona hakuna kiongozi yeyote wa ngazi ya Wilaya wala Mkoa aliye fika kuzungumza na wananchi licha ya tatizo hilo kuwa na nchi nzima.

‘Mkuu wa Wilaya ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ngazi ya wilaya vivyoi hivyo kwa Mkuu wa Mkoa ni Mwenyekiti wa Mkoa lakini tangu mgomo huo hatuja ona kiongozi yeyote kuzungumza na abiria’ alisema Mabula.

Aidha katika hatua nyingine mwenyekiti wa mawakala wa kukatisha tiketi katika kituo hicho Noah Mwakatumbula alisema kabla ya mabasi hao kuanza safari,walikutana madereva majira saa 2:30 kwa ajili ya kuwa shawishi madereva kuingia kwenye mabasi ili kuwasaidia abiria ambao walikuwa wanateseka bila hatia.

‘Tuliamua kufanya kikao ma maderva ili tuwasahiwishi lakini baadaye katika kikao tuliona tunaweza kuwaomba waondoshe magari lakini wanaweza kupata matatizo njiani hivyo tukaona ni vema kusubiri kauli ya uongozi wao wa juu’ alisema Mwakatumbula.

Aidha katika hatua nyingine alisema kuwa siyo madereva wote wanakubaliana na mgomo huo bali ni kutokana na shinikizo la viongozi wao kitaifa.

‘Siyo kila Dereva anakubaliana na mgomo kwani hili ni shinikizo hapa kuna watua wana moyo wa huruma na wapo tayari kuendesha magari ili kuwasaidia   abaria ambao wanateseka kwa siku mbili sasa lakini hofu yao huenda wakafanyiwa vitu vibaya huko mbele ya safari’ alisema Mwakatumbula

No comments:

Post a Comment

Pages