Meneja
Biashara wa Kampuni ya Udalali ya Mem, Elieza Mbwambo (kulia), akimkabidhi
funguo Meneja wa Kampuni ya Navtej Bains, Zulfiqar Hassanali, baada ya kampuni
hiyo kuwaondoa wapangaji Hospitali ya Ami waliokuwa na deni la sh. bilioni 3.2. Makabidhiano
hayo yalifanyika nje ya jengo hilo Masaki jijini Dar es Salaam, leo. (Picha na Francis Dande)
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
HOSPITALI maarufu kwa kutibu vigogo wa serikali,
African Medical Investment (AMI), hatimaye imefutwa rasmi baada ya jengo la
hospitali hiyo kukabidhiwa kwa mmiliki wa jengo hilo kwa nguvu ya mahakama.
Nao wafanyakazi wa hospitali hiyo, ambayo iko
Masaki wilayani Kinondoni, wamesema hawajui hatima yao , baada viongozi wao kuzima simu zao.
Hali hiyo ilitokana na mri ya Mahakama Kuu kuagiza
mali za hospitali hiyo
zikamatwe na jengo la hospitali hilo
lirejeshwe kwa mmiliki wake kutokana na kushindwa kulipa kodi ya pango ya sh.
bilioni 3.2 kwa zaidi ya miezi 26.
Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es
Salaam jana, Meneja wa Biashara Kampuni ya Madalali (MEM), Elieza Mbwambo,
alisema, kazi yao ilikuwa ni kukamata mali na kukabidhi jengo, masuala ya kudai
fedha ni jukumu la mmiliki.
Alisema kuwa walifikia hatua hiyo baada ya
uongozi wa hospitali hiyo kutii amri ya mahakama ya kuwaondoa wagonjwa wote na
kwamba mali
walizokamata wataziuza.
“Wiki mbili zilizopita tulikuwa hapa kukamata mali na tuliwapa taarifa wagonjwa wote waliokuwa
hapa waondoke na leo tunashukuru wagonjwa wote wameondoka na leo tunamkabidhi
jengo mwenye mali ,”alisema
Mbwambo.
Mbwambo, alisema vifaa vyote vilivyokamatwa vitauzwa,
hata hivyo, fursa itatolewa kwanza kwa mmiliki wa jengo hilo .
Akizungumza kwa niaba ya Kampuni ya Navtej Singh
ambao ndiyo wa jengo hilo , Zulfiqar Hassanali,
alisema baada ya kukabidhiwa jengo lao, wanatarajia kufungua hospitali kama
mwanzo kwa vile eneo hilo
la Msasani halina huduma hiyo zaidi hapo.
“Bado hatujampata mtu kwa sababu baada ya
kutokea tukio hilo
kuna watu wengi wamejitokeza kuomba jengo hili kwa kuendesha shughuli
hizi,”alisema Hassanali.
No comments:
Post a Comment