Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya EAG group, Zenno Ngowi
akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusu maonyesho ya tano ya Tanzania Homes Explo yatakayoanza Mei 29
katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa Masoko wa
kampuni hiyo, Hellen Mangore na Ofisa Masoko Mkuu, Richard Ryaganda. (Picha na Francis Dande)
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
ZAIDI ya Kampuni 70 hapa nchini kwa kushirikiana na nchi jirani, zinatarajiwa kushiriki katika
maonyesho ya tano ya mradi wa Tanzania Homes Expo, yatakayofanyika katika Ukumbi wa
Mlimani City jijini Dar es Salaam kuanzia kesho hadi Jumapili.
Miongoni mwa nchi
zitakazoshiriki ni Ujerumani,Uturuki,China na Kenya ambapo kwa hapa nchini kampuni zitakazoshiriki ni kampuni ya simu za mikononi, (TTCL) ,Shirika la Nyumba (NHC),
Afrikan life, Dege Village,KAFKAS na Avic Town.
Akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar esa Salaam Mkurugenzi wa Kampuni ya Eagroup, Zenno Ngowi, alisema lengo la maonyesho hayo, Tanzania Home Expo inaleta watoa huduma
mbalimbali na washauri ambao watawezesha wananchi kupata taarifa yakinifu na za
uhakika.
Alisema mchango wa sekta ya
kwenye pato la taifa ni asilimia moja tu ukilinganisha na nchi nyingine
zilizopiga hatua kwenye sekta hii ambazo zimefika asilimia 30.
“Hii inaidhinisha umuhimu wa
kuiendeleza sekta ya Nyumba, sio tu kuwapatia
wananchi makazi bali pia kuboresha maisha ya wananchi na kukuza pato la Taifa
linalotokana na sekta ya nyumba.”alisema Ngowi.
Alisema kwenye maonyesho ya mwaka huu, wametoa
uzito wa pekee kwa watoa huduma za maji hususan utakatishaji wa maji taka
,nishati mbadala na huduma za usafi wa Nyumbani,wajenzi wa nyumba pia vifaa vya
usalama wa nyumbani.
Aliongeza kuwa sekta muhimu
ambayo imekuwa chachu kubwa ya ukuaji wa sekta ya ujenzi ni mabenki na wajenzi
wa nyumba, hivyo wanategemea ushiriki mzuri wa sekta hiyo.
“Mwananchi atakayekuja kwenye
maonyesho hayo ataweza kununua kiwanja,kupata mtu wa kumchorea,kupata vifaa vya
ujenzi,kupata fedha za ujenzi na kupata nishati mbadala na ulinzi wa nyumba
yake”alisema Ngowi.
Aliongeza kuwa maonyesho hayo
yanatoa fursa kwa watoa huduma za kifedha,wakala wa ujenzi,makampuni ya nyumba
,makandarasi,mashirika ya kiserikali na wabunifu wa majengo.
No comments:
Post a Comment