HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 20, 2015

VIDEO YA 'NO BODY BUT ME' YA VANESSA MDEE YATAMBA KIMATAIFA

NA ELIZABETH JOHN


VIDEO ya wimbo wa ‘No Body But Me’ ulioimbwa na mwanadada anayetamba katika tasnia ya muziki wa Bongo, Vanessa Mdee ‘Vee Money’ aliomshirikisha rapa wa Afrika Kusini ‘K .O’ umeanza kutamba katika televisheni za Kimataifa kama Mtv Base na Trace.
Wimbo huo aliousambaza mwishoni mwa mwezi uliopita katika vituo mbalimbali vya televisheni na audio yake imeingia kwenye ‘top ten’ ya redio ya Lagos, Nigeria.
Kwa mujibu wa Vee Money, kupitia ukurasa wake wa Instagram, aliandika kuwa, anamshukuru Mungu kwa hatua hiyo aliyofikia na kwamba anahitaji sapoti zaidi ya Watanzania ili aweze kufika sehemu anayotaka.
“Nashukuru Mungu hapa nilipo, hii ni kazi yangu ya kwanza ambayo inatamba katika mataifa mbalimbali licha ya zingine kufanya vizuri, kukubwa ni sapoti kutoka kwa Watanzania wenzangu,” alisema.
Vee Money alishawahi kutamba na kazi zake kama Hawajui, Closer, Siri na nyingine.

No comments:

Post a Comment

Pages