HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 19, 2015

Lowassa apata jumla ya wadhamini 33,780 mkoani Kilimanjaro

Edward Lowassa akisaini daftari la wageni ndani na jengo la CCM mkoa wa Kilimanjaro.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza kwa wingi katika nje ya jengo la CCM mkoa mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro, June 18, 2015 alipokuja kutafuta wadhamini ambapo alipata jumla ya wadhamini 33,780 mkoani Kilimanjaro.
Kiongozi wa dini ya kiislam akimuombea Lowassa.

Kiongozi wa dini ya kikristo akimuombea Lowassa.
Edward Lowassa akiingia huku akisindikizwa na mamia ya watu mkoani Kilimanjaro.

Mheshimiwa Edward Lowassa akiwahutubia wananchi wa mkoani Kilmanjaro waliokubali kumdhamini.

Edward Lowassa akisalimiana na Lenard Minja.

Mamia ya wakazi wa mkoani Kilimanjaro waliokuja kumdhamini Edward Lowassa.
Mamia ya wakazi wa mkoani Kilimanjaro waliokuja kumdhamini Edward Lowassa.
Wakazi wa mkoani Kilimanjaro waliokuja kumdhamini Lowassa.


Na Joshua Fanuel 

KILIMANJARO, Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa aliyeianza safari ya matumaini katika uwanja wa michezo wa Sheik Amri Abeid jijini Arusha Mei 30, 2015 kwa kutangaza nia ya kuomba ridhaa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kumteua kugombea urais wa Tanzania.

Jana June 18, 2015 aliwasilili mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro kusaka wadhamini ambapo kwa taratibu za katiba mgombea anatakiwa kupata jumla ya wadhamini 450 katika mikoa 15 ya Tanzania.

Mheshimiwa Edward Lowassa amepata wadhamini  kutoka katika majimbo yafuatayo, Moshi Vijijini 11564, Rombo 6615, Hai 1854, Siha 9860, Moshi Mjini 1184, Same 1600, Mwanga 1103. Jumla ya wadhamini ni 33,780 kutoka katika mkoa wa Kilimanjaro.

Katika kuwashukuru wakazi wa mkoani Kilimanjaro waliomdhamini na wale walioacha shuhuli zao na kwenda kuungana nae katika safari ya matumaini, Lowassa alisisitiza kuwa anauchukia umasikini na akipewa ridhaa ya kuongoza nchi hii atahakikisha anatokomeza umasikini, pia aliwaahidi wakazi wa Kilimanjaro kuwa mwezi wa kwaza wa utawala wake ataanza na mkoa wa Kilimanjaro kuhakikisha amefufua viwanda vilivyofungwa ili vijana waweze kupata ajira.

Aliendelea kuwasisitizia kwa wale wenye sifa za kujiandikisha waweze kujiandikisha mapema kwenye daftari la kudumu la wapiga kura ili siku ya uchaguzi ikifika waweze kufanya maamuzi kwani wanachi ndio wenye maamuzi ya kuchagua kiongozi wanaomuhitaji.

Pia Mhesimiwa Lowassa alisema endapo atachaguliwa kuiongoza nchi ya Tanzania atahakikisha nchi nzima kuanzia viongozi mpaka wananchi wanakimbia mchakamchaka katika kufikia malengo na kwa yeyote ambaye hatakua tayari kukimbia mchaka mchaka katika kuleta mafanikio atamuweka pembeni na kupisha wale walio tayari kwa mchaka mchaka kuendelea kuijenga nchi ya Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Pages