Timu
ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro
Premium Lager, kesho inatarajiwa kushuka dimbani kucheza na timu ya
Taifa ya Uganda katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainaili za
wachezaji wa ndani CHAN 2016.
Kikosi
cha Taifa Stars kimeendelea na mazoezi katika uwanja wa Amani kisiwani
Zanzibar kujiandaa na mchezo huo utakaopigwa kuanzia majira a saa 2
usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Stars
inahitaji ushindi katika mchezo huo wa awali ili kujiweka katika
mzingira mazuri ya kusonga mbele, kabla ya mchezo wa marudaino
utakaofanyika baada ya wiki mbili jijini Kampala.
Kocha
mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij amesema vijana wake wako katika hali
nzuri kuelekea kwenye mchezo wa kesho, na kuwaomba watanzania kuwapa
sapoti katika mchezo huo.
Endapo
Stars itaitoa Uganda katika hatua ya awali, itafuzu katika hatua ya
pili ambapo itacheza dhidi ya timu ya Taifa ya Sudan, na mshindi wa
mchezo huo moja kwa moja atafuzu kwa fainali za CHAN 2016 nchini Rwanda.
Wakati
huo huo, timu ya Taifa ya Uganda (The Cranes) inatarajiwa kuwasili leo
mchana jijini Dar es salaam kisha kuelekea kisiwani Zanzibar tayari kwa
mchezo huo wa kesho dhidi ya Taifa Stars.
TWFA KUFANYA UCHAGUZI AGOSTI 15
Mwenyekiti
wa Kamati ya Uchaguzi wa Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania
(TWFA), George Mushumba ametangaza uchaguzi mkuu wa chama hicho
utakaofanyika agosti 15, 2015 kujaza nafasi mbalimbali.
Kwa
mamlaka aliyonayo anapenda kutangaza uchaguzi mkuu wa TWFA leo kwa
ajili ya kujaza nafasi zilizoachwa wazi, uchaguzi huo utafanyika tarehe
15, Agosti 2015 katika nafasi zifuatazo:
- Mwenyekiti
- Katibu Msaidizi
- Mweka Hazina
- Wajumbe wawili wa Kamati ya Utendaji.
Fomu za kuomba nafasi hizo zitaanza kutolewa tarehe 19-23 Juni 2015 katika ofisi za TFF zilizopo Karume jijini Dar es salaam.
Kalenda ya Uchaguzi wa TWFA imeambatanishwa:
JEDWALI NAMBA MOJA (1)
KALENDA YA MATUKIO YA UCHAGUZI YA TWFA
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment