HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 09, 2015

KIKAO KATI YA TFF, SIMBA SC, SPUTANZA NA MCHEZAJI SINGANO

 Ramadhani Singano 'Messi' akitoka katika Ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya kikao cha Simba na TFF kuhusu utata wa mkataba wake na Simba.
 Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Celestin akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo baada ya kikao chao na Uongozi wa Soimba pamoja na Ramadhan Singano.
 Mshambuliaji wa Ramadhan Singano na Msemaji wa Simba, Haji Manara baada ya kikao cha usuluhishi kuhusu butata wa mlkataba wa mchezji huyo.
 Ramadhan Singano akitoka katika Ofisi za TFF baada ya kikao chao.

Ramadhan Singano akitoka katika Ofisi za TFF baada ya kikao chao.
 Ramadhan Singano akiondoka katika Ofisi za TFF.

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo umekutana na Uongozi wa klabu ya Simba  SC ukiwakilishwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Collin Frisch na mchezaji Ramadhani Yahya Singano akiandamana na Uongozi wa Chama cha Wacheaji wa Mpira wa Miguu (SPUTANZA). Kikao hiki kiliitishwa na TFF kujadili utata wa kimtakabta kati ya mchezaji na klabu ya Simba.

Katika kikao cha leo pande zote zimeeleza kutambua utata ulio ndani ya mikataba iliyokuwepo ambayo kimsingi iliingiwa kabla ya uongozi wa sasa wa Simba SC.

Kwa pamoja pande hizo mbili zimekubaliana kuanza mazungumzo ya makubaliano mapya na hatimaye mkataba mpya utakaoanza katika msimu mpya wa 2015/16.

TFF imevitaka vilabu kushirikiana na SPUTANZA na Bodi ya Ligi katika kuweka mifumo mizuri ya uingiaji mikataba.  TFF inao mkataba mama (template) ambao vilabu vyote na wachezaji wanatakiwa waufuate wakati wanaandaa mikataba yao (individual contracts between players and clubs).  Aidha TFF imewataka  wachezaji kuelewa mikataba kabla ya kutia sahihi.

TFF itazidi kuboresha mfumo wa usajili wa wachezaji na mikataba ili kuweka mazingira sawia kati ya pande zote mbili (Wachezaji na vilabu)

Makubaliano yamefanyika leo tarehe 9 Juni 2015 na kusainiwa na:-
  • Collin Frisch - Simba SC
  • Ramadhan Singano - Mchezaji
  • Mussa M. Kissoky - SPUTANZA
  • Mwesigwa J. Selestine - Katibu Mkuu - TFF
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
UTATA wa mkataba wa mchezaji Ramadhani Singano na klabu yake ya Simba, jana ulipata ufumbuzi baada ya pande husika kusaini makubaliano ya kuingia katika mazungumzo mapya ya mkataba mpya kuanzia msimu wa 2015/16.

Uamuzi huo uliofikiwa jana mbele ya Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine; Simba iliwakilishwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Collin Frisch.

Wengine katika kikao hicho, ni Ramadhani Yahya Singano aliyeambatana na kiongozi wa Chama cha Wacheaji wa Mpira wa Miguu (SPUTANZA), Mussa Kissoky.

Katika kikao kiliitishwa baada ya kuibuka kwa utata wa umri wa mkataba kwani wakati Singano akisema amemaliza miaka miwili, Simba wakajenga hoja kuwa bado ana mwaka zaidi kwani mkataba wake ulikuwa wa miaka mitatu.
   
Kwa mujibu wa taarifa ya TFF, pande zote zilieleza kutambua utata ulio ndani ya mikataba iliyokuwepo ambayo kimsingi iliingiwa kabla ya uongozi wa sasa wa klabu hiyo.

“Kwa pamoja, pande hizo mbili zimekubaliana kuanza mazungumzo ya makubaliano mapya na hatimaye kusaini mkataba mpya kwa msimu mpya wa 2015/16,” ilisema taarifa ya Ofisa Habari wa Shirikisho hilo.

No comments:

Post a Comment

Pages