HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 15, 2015

KOMREDI KINANA AHITIMISHA ZIARA KAGERA,ASAFIRI KM 4884 KWA MAGARI, MITUMBWI NA MABASI

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Biharamulo leo,wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi cya chama hicho pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi. (Picha zote na Kamanda wa Matukio Blog)

Komredi Kinana ambaye katika ziara hiyo  ya Mkoa wa Kagera,ameambatana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Mnauye, ametembea kwa gari na usafiri wa mitumbwi  katika mkoa huo umbali wa Km 3,374.Pia alisafiri wa basi kutoka Dar es Salaam kwenda Bukoba kwa umbali wa km 1510.

Kinana na msafara wake wamefika katika Wilaya 8 zenye majimbo 9, ambapo amehutubia jumla ya mikutano 74, 11 ya ndani na 63 ya hadhara,Imezinduliwa jumla ya miradi 46 ikiwemo ya CCM 5 na 41 ya maendeleo.Pia wamevuna wanachama wapya 5678 wakiwemo wapinzania 488.
 Komredi Kinana akitoka kukagua mradi wa maji wa Nyakahura uliopo wilayani Biharamulo, Mkoa wa Kagera ambao umekwama kutokana na Wizara ya Maji kuwapatia zabuni ya ujenzi wakandarasi wasio faa. Mradi huo unaofadhiliwa na Benki ya Dunia kwa gharama ya sh. bil. 1.4 hadi sasa haujakamilika jambo linalotia hofu kwamba fedha za mradi huo zimeliwa badala kufanyia kazi iliyokusudiwa. Komredi Kinana ameamuru wale waote waliohusika kuhujumu mradi mradi huo wasakwe na kuwajibishwa.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akisoma moja ya mabango yaliyoshikwa na wananchi yenye maandishi ya tatizo la maji katika kijiji cha Nyakahura lililosababishwa na mradi huo wa maji usiofaa.
 Nape akihutubia katika mkutano wa hadhara na kuwaeleza wananchi kwamba kilio chao hicho wamekisikiliza na kwamba kitafanyiwa kazi.
 Komredi Kinana akihutubia katika mkutano huo, ambapo aliitaka Serikali kuwawajibisha viongozi wote waliohusika katika kuudidimiza mradi huo wa Nyakahura.
 Mkazi wa Wilaya ya Biaharamulo, Yohana Kanyahugali akioba msaada wa Seikali kwajengea shule jamii ya wafugaji na wakulima  ambao wanateseka kwa kwa kutokuwa na majengo  ya shule na kusafiri umbali mrefu kwenda shule.
 Mwenyekiti wa Umoja wa Wananwake wa CCM (UWT), Kijiji cha Busili, wilayani  Biaharamulo, Mamatandu Mniko, akilalamika mbele ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimtuhumu Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Busili kwamba ni mnyanyasaji kwa wananchi kiasi cha kuwasweka sero watu wasio na hatia, tuhuma ambazo zilizpingwa vikali na mwenyekiti wa kijiji hicho, Enock Kuhindwa ambaye alidai kuwa waliosekwa sero akiwemo mama huyo walikuwa wamefanya kosa la kutoa na kupokea rushwa ili raia wa Burundi aaandishwe katika Daftari la Wapiga kura.
 Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Busili, Enock Kuhindwa (kulia), akijibu tuhuma hizo zilozoelekezwa kwake na Mwenyenyekiti wa UWT wa  Kijiji cha Busili,Mamatandu Mniko kwamba an atabia ya unyanyasaji wananchini, tuhuma ambazo alizikana.
 Mzee Peter Kalingula, akimuomba Komredi Kinana asidie gharama za ujenzi wa majengo ya shule ya Busili na nyumba za walimu.
 Komredi Kinana akisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Meneja Umeme wa Tanesco Wilaya ya Biharamulo, Ernest Milyango kuhusu tatizo la umeme linavyotokea mara kwa mara katika wilaya hiyo wakati alipotembelea mitambo ya umeme ya Biharamulo inayotumia mafuta ya dizeli.
 Komredi Kinana akitembelea mitambo ya umeme ya Biharamulo
 Komredi Kinana akipata maelezo kutoka Mganga msaidizi wa Hospitali ya Wilaya ya Biharamulo. kuhusu ujenzi wa Wodi ya Wazazi.
 Komredi Kinana akitoka kushiriki ujenzi wa Shule ya Kiislamu ya Arahman mjini Biaharamulo
 Wnanchi wakimsalimia komredi Kinana alipokuwa akiwasili kwenye Uwanja wa Soko palipofanyika mkutano wa hadhara mjini Biaharamulo, mkoani Kagera.
 Komredi Kinana wasanii wakitumbiza katika mkutano huo.
 Nape akihutubia katika mkutano huo wa hadhara
Wananchi wakisikiliza kwa makini wakati wa mkutano huo.

No comments:

Post a Comment

Pages