Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Makongoro Mahanga (wa kwanza kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), James Rhombo tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka 2014 mara baada ya Shirika hilo na mengine mawili kutangazwa kuwa mwajiri bora wa mwaka 2015 iliyotolewa na Chama Cha Wafanyakazi wa Migodini, Ujenzi, Nishati na Kazi nyingine (TAMICO). Katikati ni Mwenyekiti wa TAMICO Taifa, Mbaraka Igangula akishihudia. Katika tuzo hizo jumla ya waajiri 160 walishindanishwa na kupatikana watatu bora ambao ni NHC, Kampuni ya kuchimba madini ya Geita Gold Mining (GGM) na Wakala wa Ujenzi wa Barabara Tanzania (Tanroad).Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), James Rhombo (Kulia) Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC, Muungano Saguya na Meneja wa Mawasiliano kwa Umma wa NHC, Yahya Charahani wakiimba wimbo wa solidarity forever wakati wa hafla hiyo.
Mwenyekiti wa TAMICO Taifa, Mbaraka Igangula akizungumza katika hafla hiyo wanaoshuhudia ni Naibu wa Kazi na Ajira, Makongoro Mahanga na Katibu Mkuu wa Tamico, Hassan Ameir.
Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC, Muungano Saguya akiwa ameshikilia tuzo ya mwajiri bora wa mwaka 2015 huku Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), James Rhombo na Katibu wa Tamico, NHC Iddi Kitete wakishuhudia.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), James Rhombo akizungumza kutoa shukurani wakati wa hafla hiyo
Picha ya pamoja
Mwenyekiti wa TAMICO Taifa, Mbaraka Igangula akizungumza katika hafla hiyo wanaoshuhudia ni Naibu wa Kazi na Ajira, Makongoro Mahanga na Katibu Mkuu wa Tamico, Hassan Ameir.
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Makongoro Mahanga (wa kwanza kulia) akikabidhi kwa Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), James Rhombo tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka 2014 mara baada ya Shirika hilo na mengine mawili kutangazwa kuwa mwajiri bora wa mwaka 2015 iliyotolewa na Chama Cha Wafanyakazi wa Migodini, Ujenzi, Nishati na Kazi nyingine (TAMICO).
Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC, Muungano Saguya akiwa ameshikilia tuzo ya mwajiri bora wa mwaka 2015 huku Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), James Rhombo na Katibu wa Tamico, NHC Iddi Kitete wakishuhudia.
...........................................
SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) limekuwa miongoni mwa waajiri bora waliopata tuzo zilizotolewa na Chama cha Wafanyakazi wa Migodini, Ujenzi, Nishati na Kazi nyingine (TAMICO).
Tuzo hizo zilitolewa mwishoni mwa wiki na chama hicho na kukabidhiwa na Naibu wa Kazi na Ajira, Makongoro Mahanga.
Katika tuzo hizo jumla ya waajiri 160 walishindanishwa na kupatikana watatu bora ambao ni NHC, Kampuni ya kuchimba madini ya Geita Gold Mining (GGM) na Wakala wa Ujenzi wa Barabara Tanzania (Tanroad).
Mwenyekiti wa Tamico Taifa, Mbaraka Igangula, alisema tukio hilo limefanyika kwa mara ya kwanza, waliamua kulibuni kutokana na kwamba siku zote wanaotunzwa ni wafanyakazi tu.
Igangula alisema hiyo itasaidia waajiri kujenga uhusiano mwema na wafanyakazi wao ambapo wakati mwingine huonekana kama paka na panya.
Alitaja baadhi ya vigezo vilivyotumika kuwapata washindi kuwa ni uhusiano mzuri na wafanyakazi, kutekeleza mikataba ya kazi, kuwepo kwa mabaraza, kushiriki kutoa michango ya kijamii na utekelezaji wa mikataba ya Shirika la Kazi Duniani (ILO).
Mwenyekiti huyo alisema matarajio yao katika kutoa tuzo hizo ni kuwa chachu ya utekelezaji wa mikataba ya kazi na mazingira wezeshi na rafiki ya
No comments:
Post a Comment