HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 22, 2015

Mamlaka ya usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) watia fola maonesho ya wiki ya Utumishi wa Umma

 Kaimu Mkurugenzi  Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) Charles Chacha  (mwenye suti) akiwa katika picha na waongoza ndege wakati alipotembelea kwenye banda la Tcaa liliopo kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Hadija Omari,Christo   Sabuni na Cosmasi Changa.
 Baadhi ya wanafunzi washule ya msingi Msasani jijini Dar es Salaam, wakijifunza  kwa kuona jinsi ya kuongoza ndege wakati walipotembelea banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA)   liliopo kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkurugenzi  Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) Charles Chacha  akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea banda la Baraza la Ushauri la watumiaji Huduma za Usafiri wa anga (TCAA-CCC) liliopo kwenye maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto   ni  Katibu Mtendaji wa Baraza Hamza Johari ,waelimishaji na wahamasishaji  wa baraza hilo Debora Mligo na Athuman Bakari.
 Kaimu Mkurugenzi  Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) Charles Chacha  (mwenye suti)  katikati akiwa katika picha na  ya Pamoja na wafanyakazi wa Baraza la Ushauri la watumiaji Huduma za Usafiri wa anga (TCAA-CCC) wakati alipotembelea kwenye banda lhilo  kwenye maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam, waliofika kwenye maadhimisho ya wiki ya utumishi wa Umma yanayofanyika kwe viwanja vya Mnazi Mmoja , wakipewa maelezo na Mwongoza ndege wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania TCAA, Hadija Omari, juu ya shughuli mbalimbali zinazofanya na TCAA ikiwemo jinsi wanaovyoweza kuongoza ndege.

No comments:

Post a Comment

Pages