HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 22, 2015

Ansaf, RCT waishauri Serikali ushuru wa mchele

Mkurugenzi Mtendaji wa Ansaf, Audax Rukonge akizungumza na waandishi wa habairi jijini Dar es Salaam, kwenye mkutano wa kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili wakulima wa mchele,
Mwenyekiti wa Baraza la Mchele Tanzania, Julius wambura akifungua semina  hiyo
Mkurugenzi Mtendaji wa Ansaf, Audax Rukonge akizungumza na waandishi wa habairi jijini Dar es Salaam, kwenye mkutano wa kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili wakulima wa mchele,
Mwenyekiti wa Baraza la Mchele Tanzania, Julius wambura akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
 Mkulima wa Mpunga kutoka Wilaya ya Mbogwe mkoani Geita akizungumza na waandishi wa habri kuhusu soko la mchele linavyoathirika na mchele wa kutoka nje.
 Washiriki wa mkutano huo. 
Slyvatus Kashanga akitoa mada kuhusu jitihada za kuboresha sekta ya Mpunga ili kulinda matarajio ya wazalishaji wa mchele wa Tanzania.

XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX


BARAZA la Mchele nchini (RCT) kwa kushirikiana na taasisi isiyo ya kiserikali inayojihusisha na masuala ya kilimo (ANSAF), wameishauri serikali kutekeleza na kuendeleza sheria ya tozo ya ushuru wa forodha ya asilimia 75 kwa mchele unaotoka nje ya Shirikisho la Afrika Mashariki ili kuwaboreshea bei wakulima wa hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kwenye mkutano wa kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili wakulima wa mchele, Mkurugenzi Mtendaji wa Ansaf, Audax Rukonge, alisema kwa kufanya hivyo kutasaidia mkulima wa hapa nchini aweze kupata bei inayoendana na uhalisia wa zao hilo.

Rukonge alisema mchele mwingi unaoingizwa hapa nchini umekuwa haulipiwi kodi, jambo linalosababisha madhara makubwa kwa mkulima, ikiwemo kushindwa kujiendeleza katika kilimo hicho na kuongeza kwamba kwa sasa mawaziri wa shirikisho hilo wapo mbioni kutaka kubadilisha ushuru huo uwe chini ya asilmia 75, jambo ambalo halikubaliki.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Mchele Tanzania (RCT), Julius Wambura, alisema serikali inatakiwa kupanua wigo wa ukusanyaji wa takwimu za bei ya mchele ili kila mwananchi aweze kupata taarifa sahihi na kwa wakati.


Kama vile haitoshi, Wambura aliomba serikali kuwezesha bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko ianze kazi ili iweze kutekeleza majukumu yake pamoja na kuweka madaraja na viwango vya ubora vinavyotakiwa kwa walaji wa mchele wa ndani na masoko ya nje.

No comments:

Post a Comment

Pages