HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 21, 2015

SERIKALI YAPIGA MARUFUKU UJENZI SLIPWAY

Na Devotha Kihwelo
SERIKALI imemtaka mmiliki wa hoteli ya Slipway kusitisha shughuli zote za ujenzi zinazoendelea pembezoni mwa bahari ya Hindi.
Akizungumza na waandishi wa habari wakili wa Baraza la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC  Manchare Heche alisema amri hiyo imetoka kwa Waziri wa Mazingira baada ya kupata taarifa kutoka kwa wananchi wanaozunguka hotel hiyo.
Alisema wamempa barua juzi kwa ajili ya kusitisha ujenzi uliokuwa unaendelea katika hoteli hiyo ya kuchukua vifusi na kuingiza baharini ili kupata nafasi kwa kuongeza majengo katika eneo la bahari.
Alisema endapo atakaidi kufanya hivyo hatua kali za kisheria zitafuata na kupelekea kuifungia kabisa kwa kutoendelea na huduma za hoteli ndani ya nchi.
“Agizo limetoka kwa waziri ili mmiliki wa hoteli hii aachane na shughuli zote za ujenzi katika eneo hiili kutokana kuwa chanzo cha uchafuzi wa mazingira na kuharibu eneo la bahari kwa kujaza mawe na vifusi vya michanga”,alisema Heche.
Aidha Heche alisema mmiliki wa hoteli hiyo anapeleka vifusi pamoja na mawe makubwa katika bahari kwa kutumia katapila pindi maji yanapohama nyakati za asubuhi.
Alisema Slipway amekiuka sheria za bahari na wizara kwa kutofuata taratibu na vibali vya kufanya hivyo na kupelekea serikali kutupiwa lawama na wananchi mabazo zinafanywa na watu wachache.
Heche alisema wamefanya hivyo iwe fundisho kwa wamiliki wote wenye tabia ya kujichukulia maamuzi kwa madai serikali haiwezo kuchukua hatua yoyote dhidi yao.
Kutokana na kitendo alichofanya mmiliki huyo cha kujaza mawe na vifusi katika bahari itaundwa kamati kwa taasisai zote zinazohusika na maswala ya bahari kwa ajili ya kujadili swala hilo na endapo hawataridhishwa na watapeleka shauri mahakamani.  
Alisema kutokana na kauli hiyo ya waziri watamfuatilia kwa karibu ili kufahamu kama bado anaendelea na shughuli hizo kwa kuwa ndio chanzo cha mafuriko katika maeneo yanayozunguka hoteli hiyo.
Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti  kwa sharti la kutotaja majina yao, wafanyabiashara wa eneo hilo  walisema  awali hawakufahamu vifusi hivyo vinakazi gani katika eneo hilo lakini waligundua kuwa vinapelekwa baharini na kushindwa kusema kwa kuhofia kufukuzwa.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake mmoja wa wamiliki wa maduka ya vitu vya asili alisema wamechoshwa na vifusi hivyo  kwa madai kuwa imekuwa shida pindi mvua zinaponyesha kwani hukosekana sehemu ya kupita kutokana na tope pamoja na maji kutuama katika njia za maduka yao.
 “Kwakweli maeneo haya imekuwa kero kwa ajili ya vifusi pamoja na magari yanayo  kushusha  kukosa njia pindi mvua zinaponyesha na sio sisi tu hata majiranai na watalii wanaokuja hapa wamekuwa na wakati mgumu sana pindi mvua zinapo nyesha”.Alisema mmoja wa watu hao.
Gazeti hili lilipojaribu kumtafuta mwanasheria wa hoteli hiyo kuzungumzia swala hili halkipokea simu na mwisho akazima kwa kuondoa usumbufu.

2 comments:

  1. Its like you read my mind! You seem to know a lot about this, like you wrote the book in it or something.
    I think that you can do with a few pics to drive the message home a little
    bit, but other than that, this is great blog. A great read.
    I will certainly be back.

    Feel free to visit my website ... lasertest

    ReplyDelete
  2. Gorgeous! That you don't come by information similar to this simply and
    I am not so ungrateful! Keep it-up men!

    ReplyDelete

Pages