HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 21, 2015

UTT AMIS ILIVYOSHIRIKI MAONYESHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2015

Ofisa Mafunzo Idara ya Masoko UTT AMIS, Waziri Ramadhani (kulia) akitoa maelezo ya namna ya kujiunga na Mfuko wa Umoja wakati wa maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Ofisa Mafunzo Idara ya Masoko UTT AMIS, Waziri Ramadhani (kulia) akitoa maelezo ya namna ya kujiunga na
Mfuko wa Umoja wakati wa maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Kulia ni Ofisa wa Mafunzo wa UTT AMIS, Doris Malenge.
Mmoja wa Wateja waliotembelea banda la UTT AMIS akijaza fomu kwa ajili ya Mfuko wa Watoto kwenye maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma jijini Dar es Salaam. Kulia ni Ofisa Msaidizi wa Huduma kwa Wateja, Saidi Mkomwa.
Maofisa wa UTT AMIS wakiwa katika picha ya pamoja. Wa pili kulia ni Ofisa Masoko Mwandamizi, Martha Mashiku, kulia ni  Ofisa Msaidizi wa Huduma kwa Wateja, Saidi Mkomwa, Ofisa Uendeshaji UTT AMIS, Justine Joseph (kushoto) na Ofisa Mafunzo, Doris Mlenge (wa pili kushoto) na Ofisa Mafunzo Idara ya Masoko, Waziri Ramadhani (katikati).

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx


Kampuni ya Uwekezaji ya UTT Asset Management and Inventor Services Plc (UTT AMIS) ni mrithi wa taasisi ambayo hapo awali ilijulikana  kama Dhamana ya Uwekezaji Tanzania (UTT), ambayoiliundwa  Juni 19, 2003.

UTT AMIS ni taasisi ya serikali chini ya Wizara ya Fedha ambayo kuanzia mwezi Julai 2013 imechukua na kusimamia kazi zote za iliyokuwa UTT.

Dhumuni kuu ni kuazisha na kuendesha mifuko ya uwekezaji wa pamoja ili kuwawezesha wananchi kujiwekea akiba huku wakiwekeza katika Masoko ya Mitaji na Fedha. Hadi sasa UTT AMIS inaendesha mifuko mitano, ambayo ni Mfuko wa Umoja, Mfuko wa Wekeza Maisha, Mfuko wa Watoto, Mfuko wa Kujikimu na Mfuko wa Ukwasi.

No comments:

Post a Comment

Pages