Kamati ya
Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika kikao chake cha
leo pamoja na mambo mengine kilipitia mwenendo wa timu ya Taifa (Taifa Stars)
ikiwa ni pamoja na kuhudhuria mchezo kati ya Tanzania na Uganda, kama sehemu ya
tathmini ya mwenendo wa timu.
Kamati ya
Utendaji kwa kauli moja imeamua yafuatayo;
1. Ajira ya
Kocha Mkuu Maart Nooij (pichani) imesitishwa mara moja kuanzia Juni 21, 2015.
2. Benchi lote
la ufundi la Taifa Stars limevunjwa kuanzia Juni 21, 2015.
3. Uongozi wa
TFF utatangaza punde benchi jipya la ufundi la timu ya Taifa.
No comments:
Post a Comment